BENCHI la ufundi la Namungo limefunguka kuwa majeraha ya straika wao, Relliants Lusajo ndio yaliyomkwamisha kwa msimu huu kufanya vizuri kwenye ligi.

Lusajo kwa msimu huu amefanikiwa kufunga mabao 10 na kufanikiwa kutoa assisti sita. Pia amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Namungo kwa msimu, magoli yake yameisaidia timu hiyo kumaliza nafasi ya tano kwa kujikusanyia alama 41.

Namungo, Majeraha Yanavyomkwamisha Straika Namungo, Meridianbet
Kocha Msaidizi wa Namungo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema kuwa “Lusajo ni mshambuliaji bora wa Tanzania na timu ya taifa hivyo ataendelea kuwa bora.
“Kilichomkwamisha msimu huu ni majeraha ya misuli aliyokuwa nayo, kama mnakumbuka aliitwa kwenye timu ya taifa lakini alishindwa kujiunga na timu hivyo huenda angekuwa bora sana.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa