Mshambuliaji nyota wa klabu ya Yanga Fiston Mayele, je huu ndio msimu wake wa mwisho na mabingwa wa Tanzania bara wa NBC Premier League?
Awali kulikuwa na taarifa kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa kutokea nchini Congo kuwa amesajiriwa na klabu inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini Kaizer Chief, lakini kulikuwa hakuna uthibitisho wowote zaidi ya taarifa kutoka kwa mwandishi kutokea nchini Ghana Nuhu Adams.
“Mshambuliaji Fiston Kalala Mayele (28) amesaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya kaizer Chief na atatangazwa hivi karibuni. Fiston anashika nafasi ya pili kwa ufungaji kwenye ligi kuu ya tanzania akiwa na magoli 16. Twende sasa.” Aliandika Nuhu Adams kwenye ukarasa wake wa Twiiter june 30.
Leo mzee wa kutetema alichapisha kwenye mitandao ya kijamii kuishikuru Tanzania na kuwaaga
“Asante Tanzania, tutaonana.”
https://twitter.com/IamFistonMayele/status/1545068343773765637