Ninavyomuona Neymar, Natafakari tu Akitundika Daluga Itakuaje?

Ni kweli Neymar Jr anatupenda? Binafsi naona ni mapenzi ya mashaka, kaamua kutupa pesa wakati amelewa, pesa hii tuna hofu ya kuitumia kwakuwa ni mlevi huenda kesho akaamka na kutudai pesa yake, nina wasiwasi moyoni

Neymar katukopesha mabao 61 kwenye mechi 101 pale Brazil, anamfukuzia Pele mwenye mabao 77, pale Barcelona kapiga mabao 105 na Assists 77 kwa mechi 186 tu ila PSG kaweka mabao 69 kwenye mechi 80 na Assists 39, ni takwimu bora sana ila najua kalewa nahofia sana kujidai kijiweni

Neymar Jr

Tukitaka kujua kuna umbali gani kati ya jana na kesho hapo ndipo moyo wangu unateseka zaidi, Neymar leo atamka mzima ila jioni ataumia, tutamkosa Kijiweni kwetu kwa siku nyingi, Neymar leo atakua sawa ila kesho atampiga mtoto wa Mjumbe wa mtaa kisha atapelekwa rumande, hatabiriki huyu, jana na kesho ipo kichwani mwake, Nidhamu tatizo

Lakini vipi kuhusu kumbukumbu atakazotuachia fundi huyu kutoka mitaa ya Mogi da Cruzes pale Sao Paulo?? Binafsi nawaambia wanangu Kijiweni bila wasiwasi naona Neymar anaturudisha kule tusipotaka kukumbuka

Anatukumbusha Andy Van der Meyde, yule fundi winger wa Ajax watu walishakesha Bar kusifia kipaji chake, pale Amsterdam ukitaja jina lake hivi sasa wanaishia kulia tu, Fundi aliishia kula unga na bangi, Neymar atatuachaje wanangu hapa Kijiweni??

Neymar huenda akatuacha na stori kama ya Ricardo Quaresma, fundi wa Kireno aliyekubali kuondoka Barcelona kumpisha Deco, aliamua kutukosesha ladha yake, na vipi kuhusu Adrian Mutu fundi wa Romania??

Siku Neymar akitangaza kutundika daruga atatuachaje, inauma sana kumpenda mtu ambaye hatupendi,

40 Komentara

    Neymar anaonekana ni mtu wa starehe Sana Sasa atakapotundika daluga ataendelea kutumia pesa mpaka atafilisika,

    Jibu

    anapesa nyingi ndomana anazigawa,ila ipo siku atazikumbuka izo pesa anazozitupa

    Jibu

    Pesa nyingi ndomana anazimwaga

    Jibu

    Atajua yy na sifa zake

    Jibu

    Naymar anaonekana ni mtu wa starehe

    Jibu

    Watu wrote awawez kufanana

    Jibu

    Itakuwa ni mapema mno kwa yeye kufanya maamuzi hayo lakini si ajabu kwa wachezaji wanaotokea america kusini uwa wanaendekeza sana starehe

    Jibu

    Kutoa ni moyo mwacheni agawe.

    Jibu

    Neymar anapenda sifa saana..

    Jibu

    Duuh Neymar mtu mbaya 😀😀😀😀😀😀😀

    Jibu

    Ni mapema sana kwa yy kufanya maamuzi hayo

    Jibu

    Neymar ni mchezaji mzuri Sana shida yake anapenda Sana ubishoo

    Jibu

    Ni maoni ya mwandishi ila kama itatokea ivyo basi atabaki kwenye vichwa vyetu kama mchezaji mahili na aliyejaribu kuvunja rekodi ya pele japokuwa anaweza kuvunja sababu muda bdo anao

    Jibu

    tatizo la neymar ubishoo umemjaa

    Jibu

    Ni pesa zake na matumizi ni yake haina shida hata kama akizigawa au akiwa na matumizi mabaya

    Jibu

    Hawezi kuwaacha kama mnavodhani Kwani neymar hapendi mashabiki wake ?anawapenda sana hawezi kuwaangusha.

    Jibu

    Duuuh

    Jibu

    Kaiacha tuzo yake ya mchezaji bora Barca kafauta pesa huyu fundi wa mpira

    Jibu

    Ndo hivyo tena tupambane na hali zetu#Meridianbettz

    Jibu

    neymar yuko poa ila ubishoo ndo unamkost yaonekana kama vile mtu mwenye kupenda sana mshahara kuliko kaz

    Jibu

    neymar yuko vizur ila Tatizo ubishoo starehe zimemzidi sana

    Jibu

    Huyo Neymar starehe zimemtawala cha msingi achague moja….starehe ama kazi

    Jibu

    Neymar n mchezaji mzur ila starehe zimemzid

    Jibu

    Neymar yupo vizuri anajua ila anapokwenda Sasa sipo atakifanya kipaji chake kishuke naizo pesa zake Zita muweka pabaya asipo angalia atajiweka sehemu mbaya

    Jibu

    Neymar atatuachaje wanangu hapa Kijiweni#meridianbettz

    Jibu

    Sidhani kama hayo maneno yana ukweli..

    Jibu

    Tatizo anapenda starehe sana kuliko mpira.

    Jibu

    Neymar ni mchezaji mzuri Sana Ila tatizo mtu wa Bata Sana#meridianbettz

    Jibu

    Neymar atakuwa na matumizi mbaya ya fedha zake kwa maana amezipata kwa njia ya ulaghai

    Jibu

    Tatizo la Wabrazil wengi ni kupenda starehe wakishaanza kupata fedha#meridianbettz

    Jibu

    huyu Neymar mpira umeshakwisha hakuna chochote zaid ya kuuza,sura na kucheza,na majukwaa

    Jibu

    Shda Neymar jr kaacha kucheza mpr ulaya kaenda kutafut pesa Ila bdo ni fundi wa mpr

    Jibu

    Ni mchezaji mzuri ila majeraha ya Mara kwa mara ndo maisha yake kwenye career yake

    Jibu

    Ukweli ni kwamba Neymar ni Talented player na amefanya mambo makubwa lakini kuna vitu vitamfanya asiweke alama kubwa kama wa Brazil wengine.

    Jibu

    Talent player

    Jibu

    Neymar ni mzuri anajua kuucheza mpira shida ubishoo na sifa ndo zinamponzaga

    Jibu

    Ni mchezaji mzr lkn bishoo,anaweza kucheza mpira mwenye kiwango km Cha Messi na Ronardo

    Jibu

    Neymar ubishoo utamfanya apotee mapema kwenye soka

    Jibu

    Binafsi nawaambia wanangu Kijiweni bila wasiwasi naona Neymar anaturudisha kule tusipotaka kukumbuka mana wakali wetu wote wamestahafu na umri umewapa mkono neymar namkubali sana

    Jibu

    Ameumis uwanja akikanyaga nyasi naona atakiwasha baraa

    Jibu

Acha ujumbe