Jurgen Klopp Alivyoacha Alama Kila Mahali Alipokanyaga

Jurgen Klopp huyu ni mkombozi wa mbalii anatoka ng’ambo kuja kusaidia watu , kama vile alivotumwa Musa kukomboa wana wa Israel kutoka utawala wa kimabavu pale Misri chini ya mtawala Farao . Kama vile Sam Allardyce au Big Sam yeye ni mkombozi maarufu pale England ajira zake ni maarufu saana mwanzoni mwa mzunguko wa pili , wale walio dhohofu sanaa kushuka daraja hili ndo kimbilio lao . Roberto Di Matteo nae alikua mkombozi wa mbali , alikuja akaichukua timu kutoka shimoni akaipa UEFA na Fa , hawa ni wakombozi huwa wanakuja wanakupa kitu wanasepa , kumpa Big Sam msimu mzima sio nzuri kiafya.

Jurgen Klopp

Jurgen Klopp huyu ndie mkombozi wa Ng’ambo mwingine , huyu ndie mkombozi anayependwa zaidii duniani yaani ni mkombozi asiye na makuu pia ambaye hana gharama . Mkombozi asiye na kelele na akiondoka lazima mtamlilia lakini atakwenda na hatarudi , mikono ya kwaheri itamtoa machozi na vilio vya mashabiki vitamuumiza lakini atakwenda na wala hatarudi . Unaweza usielewe lakini angalia jinsi mashabiki na wachezaji wa FSV Mainz 05 walivyolia kwa uchungu sanaa , angalia ambavyo Dortmund walivyomlilia siku ya kuondoka . Rais wa Borrusia Dortmund Reinhard Rauball aliwahi nukuliwa akisema moja ya vitu wanavyojutia ni kumruhusu Jurgen Klopp aende….

Baada ya kuitumikia kwa muda mrefu timu ya FSV Mainz 05 kama mchezaji , lakini mwa 2004 aliipandisha timu hiyo daraja kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu yao . Licha ya udogo wa klabu hiyo , udogo wa uwanja pia hawana hela lakini Klopp alifanya Mainz iwe tishio Bundersliga pia aliiwezesha kufuzu michuano ya Europa kabla ya kutolewa hatua za mwanzoni kabisa na Sevilla . Timu ilivoshuka daraja aliamua kubaki nayo , lakini alivoshindwa kuipandisha akaamua kuachana nayo , wakazi na wazawa na mashabiki wa klabu na jiji la Mainz walilia kilio kisicho na mwisho . Mkombozi aliamua kuondoka alifunga vioo na kuvaa miwani….

Mkombozi kutoka ng’ambo aliamua kutafuta mnyonge mwingine amsaidie akaibukia Dortmund , Thomas Doll alioneshwa mlango wa kutokea baada ya kumaliza nafasi ya 13 safari ya mafanikio ikaanza rasmi . Klopp aliamua kuitengeneza Dortmund kuwa tishio barani ulaya achana na ile ile back to back pale Bundersliga mbele ya vigogo Buyern Munich , mkombozi aliamini saana katika vijana na waliampa matunda . Mario Gotze , Nuri Sahin , Marco Reus ,Matts Hummels , Neven Subotic , Roberto Lewandowski na vijana wengine wengii . Baada miaka nane mkombozi alikwenda huku akiacha alama kubwa sanaa pale Borrusia Dortmund walimlilia lakini ndo alikwenda ivo hakuwaza kurudi.

Jurgen Klopp

Mwaka 2015 aliingia makubaliano kwenda kuifundisha Liverpool , mkombozi wa ng’ambo alilidhika na project ya mmiliki wa Liverpool na John Henry aliamua kuingia mkataba wa miaka mitatu . Aliitengeneza Liverpool kwenda kua moja na timu hatari duniani msimu wake wa kwanza aliingia fainali mbili japo hakushinda , miaka inavyokwenda mkombozi alionesha mwanga taratibu alianza kujijengea utawala pale , msimu uliofuata aliingia big four tena unaofuata akaingia fainali ya UEFA na Real Madrid kabla ya uzembe na uchawi wa golikipa Lorris Karius walirudi mikono mitupu . Na sasa anaenda kufanya kitu ambacho kilishindwa kufanyika ndani miaka takribani miaka 30 , Klopp hajawahi angushwa na wamiliki hasa linapokuja swala la bajeti kwani huwa hakurupuki , inaonekana mke wa mmiliki wa Liverpool Linda Pizzuti Henry wakati wa ngololo huwa anabana kwa juu mpaka mzee hawi mchache na mvivu kwenye bajeti.

Mkombozi anakwenda kutengeneza kilio kingine , ipo siku atamwaga watu machozi watamlilia lakini atakwenda na hatarudi . Kila palipo na harufu ya Liverpool Klopp anasemwa na anapendwa kuanzia uwanjani mpaka maisha ya kawaida , kuanzia Melwood hadi Anfield jamaa anapendwa sanaa . EPL ya kihistoria anayoenda kuwapa hawatamsahau kamwe kama walivyoshindwa kuwasahau Bill Shankly na Bob Paisley . Siku anayoondoka tutashuhudia mengi saana.

41 Komentara

    Alama kubwa ameiweka na ataendelea kuweka Kama ataendelea kuwepo pale EPL

    Jibu

    Story ya kuvutia sana, Jürgen Clopp ni Kocha na mhamasishaji mzuri. Nataka kuona kama msimu huu ataipa Liverpool Ubingwa baada ya kuukosa kwa miaka 30#meridianbettz

    Jibu

    jurgen endelea kuwa na moyo huo huo

    Jibu

    Jurgen clopp nikocha muhamasishaji

    Jibu

    Big up to jurgen

    Jibu

    Nategemea maajabu kwenye msimu huu

    Jibu

    Jurgen ameiweka na Kama ataendelea kuwepo pole EPL

    Jibu

    Tunategemea afanye maajabu Kama ataendelea kuepo

    Jibu

    Klopp the master ni kocha ambaye klabu zote duniani zitajivunia kufanya kazi pamoja na yeye

    Jibu

    Juegen klopp ni kocha anaejua

    Jibu

    Clopp ni kocha mzuri sana ndo maana hupendwa na wengi

    Jibu

    Klopp kocha mahiri saana..

    Jibu

    Nataka nione kama ataipa ubingwa Liverpool baada ya kuukosa zaidi ya miaka 30 iliyopita

    Jibu

    Jurgen aendelee kuwa na moyo huohuo

    Jibu

    Mwandishi yuko sahihi sana kumuita mkomboz, mana ameenda kuikomboa liverpool baada ya miaka 30

    Jibu

    Namkubali Sana Mana ni kocha anejua kupanga mashambulizi kwa wachezaji wake

    Jibu

    kocha mwaijibikaji

    Jibu

    Duuh! Nimependa sana Jurgen Klopp jinsi anaviishi kiuharisia kuanzia maisha ya kawaida mpka uwanjani ,anafaa kuigwa na kila mtu mwenye malengo.

    Jibu

    Inapendeza sana kama ukiacha alama nzuri sehemu na watu wakaendelea kukukumbuka big up kwake

    Jibu

    Habari njema sana hii

    Jibu

    Habari mjema

    Jibu

    binafsi machozi yatanidondoka ….YNWA tunashukuru ameongeza mitatu mingine..Klopp is Kop

    Jibu

    Kweli anapaswa kuliliwa #Meridianbettz

    Jibu

    Jurgen klopp yuko vema sana namkubali

    Jibu

    Habari njema sana hii

    Jibu

    Still bado klopp n kocha mzur sana tnx # meridianbettz

    Jibu

    Jurgen Klopp yupo vizuri tumpe pongez zake kwakweri

    Jibu

    Klopp hajawahi angushwa na wamiliki hasa linapokuja swala la bajeti kwani huwa hakurupuki

    Jibu

    Huyu jamaa ni kocha mzuri sana.

    Jibu

    Jurden Klopp ni mtu Mzuri sana

    Jibu

    klopp ni bonge la kocha ambaye anafit kwenye mifumo yote kwa sasa

    Jibu

    Bonge la Coach.. klopp fundi wa mbinu katika uwanja#meridianbettz

    Jibu

    amefanya mambo makubwa sana pale liverpool na EPL kwa ujumla ndio maana kila sehemu kaacha alama

    Jibu

    Klop namkumbali ni kocha mzuri sana

    Jibu

    Klop ni kocha bora sana katika karne hii

    Jibu

    Klopp ni moja Kati ya makocha Bora hv hv Sasa ulaya na dunia na mipaka yake

    Jibu

    Ni kocha mzuri sana na anambinu zote katika mpira

    Jibu

    Klopp alikuwa mahili mzuri ndo maana kila alipokuwa anakanyaga aliacha alama nzuri

    Jibu

    Klopp ni kocha mzuri,anajua kuishi na wachezaji ndio maana Kila anapopita anaacha alama

    Jibu

    Ni kocha wa tofaut mwenye upeo tofaut wa kuona mbali

    Jibu

    Klopp ni kocha makini sana anajua kuibua vipaji anajua kumkomaza mchezaji

    Jibu

Acha ujumbe