Mwalimu wa timu ya taifa ya Brazil Adenor Leonardo Bacchi maarufu kama Tite ametangaza kikosi chake kitakachoenda kupeperusha bendera ya taifa hilo kwenye michuano ya kombe la dunia.

Jana majira ya saa moja kamili usiku kocha huyo alitangaza kikosi chake chenye jumla ya wachezaji 26, kwenye taifa hilo ambalo limekua likileta changamoto zaidi wakati wa kuchagua timu kuelekea michuano mikubwa.BRAZILKikosi cha mwalimu Tite cha wachezaji 26 kilichoitwa ni kama ifuatavyo Makipa Alisson Becker Liverpool, Ederson Manchester City, Weverton Palmeiras Mabeki Dani Alves Pumas,Danilo Juventus, Alex Sandro, Alex Telles, Bremer Juventus, Eder Militao Real Madrid, Marquinhos PSG, Thiago Silva Chelsea Viungo Lucas Paqueta West Ham, Bruno Guimairaes Newcastle, Casemiro Manchester United, Everton Ribeiro Flamengo, Fabinho Liverpool, Fred Manchester United Washambuliaji Antony Manchester United, Gabriel Jesus, Gabriel Martinelli wote Arsenal Pedro Flamengo, Raphinha Barcelona, Richarlison Tottenham, Rodrygo, Vinicius Jr wote Real madrid, Neymar PSG

Kama ilivyo kawaida kwa timu ya taifa yeyote wakati wa kuchagua timu lawama hua hazikosekani, na ndicho kilichotokea baada ya kikosi cha Brazil kutangazwa jana ambapo watu wameshangazwa kutokuitwa kwa mshambuliaji wa Liverpool Roberto Firmino.BRAZILLakini pia kuna wachezaji ambao ilionekana watakosa nafasi kwenye kikosi hicho lakini wamepata nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha taifa hilo kama Gabriel Martinelli, pamoja mshambuliaji Gabriel Jesus wote kutoka klabu ya Arsenal ya ligi kuu ya Uingereza.

Jambo la kushangaza zaidi ni kuitwa kwa beki wa kulia wa klabu ya Fc Barcelona Dani Alves mwenye umri wa miaka 38,Wakati huu akiwa hachezi mpira kwenye kiwango cha juu wala klabu kubwa ulaya lakini anepata nafasi ya kuiwakilisha timu ya taifa ya Brazil.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa