Ulinzi Qatar Waimarishwa Kuelekea Kuanza kwa WC

Askari wa kutuliza ghasia wa Ufaransa waliohusika na kufyatua mabomu ya machozi kwa mashabiki wa Liverpool, na kikosi maalum cha Uturuki wataandaliwa kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia la Qatar katika jitihada za kuzuia vurugu za soka.

Maafisa kutoka kote ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na Uingereza, Marekani, Uturuki, Korea Kusini, Ufaransa, Italia na Pakistan, ni miongoni mwa muungano unaotarajiwa kuwasili katika taifa hilo la Ghuba huku ukijiandaa kukaribisha wageni milioni 1.2 wakati wa mashindano hayo ya kimataifa.

 

Ulinzi Qatar Waimarishwa Kuelekea Kuanza kwa WC

Maafisa hao wa ziada watatumwa katika viwanja vinane vya michezo katika mji mkuu wa Qatar, Doha, na pia katika hoteli ambazo timu 32 zitakazochuana zitakuwa zikikaa.

“Operesheni Ngao ya Kombe la Dunia” ambayo imepewa jina itashuhudia baadhi ya vitengo vikali zaidi vya polisi vilivyoundwa, ikiwa ni pamoja na kitengo cha operesheni maalum cha Uturuki, Polis-Özel-Harekat.

Maafisa hao maalum wa Uturuki mara nyingi hutumiwa kupambana na ugaidi lakini wamekuwa wakichunguzwa kwa ukiukaji wao wa haki za binadamu. Lakini kuja Kombe la Dunia, kikosi cha askari 100 kitakuwa na bunduki, magari yenye silaha na helikopta ya mashambulizi.

 

Ulinzi Qatar Waimarishwa Kuelekea Kuanza kwa WC

Chini ya itifaki iliyotiwa saini kati ya nchi hizo mbili na kuchapishwa katika gazeti rasmi la serikali ya Uturuki, taifa hilo pia linatuma polisi 3,000 wa kutuliza ghasia, wataalamu 50 wa mabomu na 80 wa kunusa na mbwa wa kutuliza ghasia.

Pia wamejitolea kutuma meli yao ya kivita, TCG Burgazad, katika jitihada za kuimarisha usalama katika Kombe la Dunia. Meli hiyo pamoja na maafisa 250 tayari wametumwa Doha katika mwezi uliopita kwa maandalizi ya kuanza kwa Kombe la Dunia mnamo Novemba 20.

Uturuki pia itakuwa inashughulikia ulinzi wa kemikali, kibaolojia, radiolojia na nyuklia wakati mashindano hayo yakiendelea.

 

Ulinzi Qatar Waimarishwa Kuelekea Kuanza kwa WC

Chanzo kimoja kilifichua kuwa wamekuwa wakijifunza Kiingereza na kwamba maafisa wa Qatar hawataweza kuwapa maagizo ya moja kwa moja.

Takriban Waqatari 800 pia wamefunzwa na Uturuki kuhusu masuala kuanzia ‘usalama wa michezo’ hadi ‘kuingilia matukio ya kijamii’, chanzo hicho kiliongeza.


aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.