Baada ya kusitishwa kwa muda mrefu kutokana na janga la virusi vya corona, La Liga inarejea viwanjani Alhamisi ya leo, Juni 11 kwa mechi kali kati ya Sevilla ikikabiliana na Real Betis kwenye Seville Derby, na michezo mingi ikifatia wikendi hii ikiwa ni pamoja na Barcelona vs Leganes (Juni 16) na Real Madrid vs Valencia (Juni 18).
Vita ya Ubingwa: Barcelona wanaweza kutetea Ubingwa?
Barca wana faida mbili wakati watakaporejea kupigania taji la La Liga kwa mara ya tatu mfululizo Jumamosi hii na mechi ya kwanza wanasafari kuwafata Mallorca.

Jambo la kwanza; Barca wanaanza raundi ya kukamilisha michezo 11 ya mwisho Ligi, wakiongoza msimamo kwa tofauti ya pointi mbili juu ya Real Madrid. Faida ya pili waliyonayo ni kwamba nahodha Lionel Messi yuko fit, kinara wa mabao wa ligi (19) na mtoaji assists nyingi zaidi (12). Ikumbukwe pia Katika misimu 10 kati ya 15 iliyopita, timu iliyo na Messi imeshinda taji la La Liga.
Barca pia ina changamoto; Hakuna imani kubwa Barca wataweza kushinda michezo yote 11 iliyobaki. Bado wanamechi ngumu. Watacheza ugenini dhidi ya Sevilla na Villarreal, timu ambazo zimewamesumbua kwa miaka ya hivi karibuni, wakati huohuo wanamichezo migumu ya nyumbani dhidi ya Athletic Bilbao na Atletico Madrid. Pia kuna Derby ya Kikatalani dhidi ya Espanyol huko Camp Nou.
Nafasi ya Real Madrid kubeba taji?
Kuna jina moja linatosha kuelezea ni kwanini Real Madrid wanaamini wanaweza kuipita Barcelona na kubeba taji: Eden Hazard.

Msimu wake wa kwanza umeanza kwa kusuasua kutokana na kuwasili Real akiwa ameongeza uzito (Kibonge) pia majeraha ya mara kwa mara. Lakini kwasasa Ripoti kutoka Madrid zinasema makali yake yamereja kuanzia mazoezi huko anamshangaza kila mtu, hat trick kwenye mechi ya mazoezi.
Hazard hayuko peke yake, pia kuna Marco Asensio yuko fit – winga Gareth Bale amerejea katika kikosi akiwa fit zaidi kuliko mchezaji mwingune yoyote wa Real baada ya vipimo vya mwili mazoezini na anapaswa kufurahia kucheza bila kusikia filimbi za kuzomewa na mashabiki.


warda
Mambo ipo huku sasa daaa!Hadi raha#Meridianbettz
Adelta
Mambo Ni Moto
Ester jackson
Pongezi sana bale hukujiachia kwa kipindi cha corona sasa funga mkanda kaza buti uwe bora zaidi
Aziza mushi
Asanteni kwa taarifaa
Rehema
Eeeeh bwanaee Safi sn meridianbet Leo mmenipa raha bonge la makala big up meridianbet
Devotha
Hiyo vita mshindi naona atakua Barca😊#meridianbettz
Mwanaidi
Asante meridian kwa makala
Elika
Hatimaye miamba 2inakutana leo ..baada ya janga la dunia
Zeiyana
Harakati za kuwatafuta mabingwa ushaanza..!tunatarajia mabadiliko
Khadija
Duuh hii kweli noma sana##meridianbettz
Neema juma
Mambo sasa yameivaa rasmi
Magdalena
Atashinda Barcelona
isha
hapo sijui bingwa atakua nani
Ernest
Nadhani msimu huu utakuwa wa namna yake katika harakati za kukimbiza ubingwa kati ya mahasimu hawa wawili
mwakalosi
mwanzo kabisa tunaanza na darby ila katika hii darby sevila anashinda
Neema hassan
Barcelona ushindi lazima
Samiah
Ushindi kwa madridi
Samira
Mambo yanazidi kuwa matamu😏😏
Johnmary joel
Jamani habari hizi zina furahisha#meridianbett
Emmy cleopa
Ahsante kwa taarifa
Amiri Kayera
Msimu wa Real Madrid kuchukua Ubingwa#meridianbettz
Hamidu
Tusubiri na tuone!
Sylvester
Wababe wa soka wanarejea sasa itakua ni uhondo juu ya uhondo#meridianbettz
Theckla
Patakuwa hapatoshi
Mwanahamisi
Ushindi kwa barcelona
Tahiya
Ni patashika uko laliga kwenye mbio za ubingwa mchuano apo ni mkali
Mwajuma
Madrid ndio mpango mzima
Povel
Msimu huu utakuwah wa kibabe sana thnks meridian bet kwa update za michezo
Rehema Dickson
Msimu huu mambo yatakua makubwa sana zaidi ya sana
Agness
Tunawasubiri kwa ham
Mwanahamisi
Ushindi kwa barcelona
Antony Luseno
Subiri adi ligi itakapoisha tuone mbabe ni nani
Gabriel
Mambo n Moto ila kwa msimu huu Barcelona inatakiwa ijipange ukiangalia juu ya usajil wa Madrid wako vizur sana na kocha wao zinedine Zidane n mzoefu
Lydia Emmanuel Magoti
Tusubili mpaka ligi itakapo Isha tuone nani mbabe
Furahav
Ligi ya hispain naikubali sana.
Theonestina
Baca ushindi lazima
Genia Sikaluzwe
Patakuwa hapatoshi
Shafii
Wapinzani wa jadi hao wa laliga napenda Sana
Frank Patrick
La liga ipo patamuu
Salma
Patachimbika
Hamidu
Burudani imerudi ! Tukae mkao kupiga pesa#meridianbettz
lombo
Lliga imepamba moto habar njema
felister
piga kelele kwa real ake 🎷🎷🎷
Ester mmakasa
Ni nzuri sana hii burudani ndani ya burudani.
Dorophina
Patakuwa hapatoshi kwenye vibanda umiza watu km wote
Caroline
Madrid lazima ashinde
David Pere
Yani hapo atayepoteza mechi moja ashakosa ubingwa
Asia Abdy
Nasubiri kwa hamu
Isaya massawe
No hatari sana tunasubir tuone nani atautwaa ubingwa