Kwa Nini Schalke Wamemtimua Manuel Baum?

Schalke wanamtafuta kocha wao mkuu wa tatu wa msimu huu baada ya kutangaza kumfuta Manuel Baum.

Baum aliteuliwa na Schalke mwezi Septemba 30 kufuatia David Wagner kufungishwa virago, ambaye alipoteza kazi yake baada ya michezo miwili kwenye ligi ya Bundesliga.

Bosi wa zamani wa Augsburg Baum hakuweza kubadilisha fomu mbaya ya klabu, hata hivyo, ameshindwa kufanya vizuri baada ya kupokea vipigo sita na sare nne katika mechi zake 10 za ligi.

Schalke Yamtimua Kocha Manuel Baum.

Baada ya kupoteza mchezo wa Jumatano 2-0 nyumbani dhidi ya Freiburg, Schalke yupo mkiani akiwa amekusanya alama nne pekee.

Schalke alithibitisha habari hiyo kwenye tovuti yao rasmi siku ya Ijumaa na kuongeza kuwa mjumbe wa bodi Huub Stevens atabeba mikoba ya kuisimamia kwa muda kwa michezo miwili iliyobaki ya 2020, na Mike Buskens ametajwa kuwa msaidizi wake.

Royal Blues haijapata ushindi katika mechi 28 za ligi na itakabiliwa na Arminia Bielefeld ambao wapo nafasi 16 msimamo siku ya Jumamosi, kabla ya kusafiri kwenda SSV Ulm katika raundi mbili za DFB-Pokal Jumanne ijayo.

Sehemu ya taarifa ya klabu ina ujumbe huu:

“Mchezo wa nyumbani dhidi ya Arminia Bielefeld ni muhimu sana kwa klabu yetu,” mkurugenzi wa Schalke Jochen Schneider alisema katika taarifa.

“Kiwango cha kukatisha tamaa dhidi ya Freiburg kilituonyesha kwamba timu inahitaji msukumo mpya ili kuweza kucheza michezo ijayo kwa mafanikio.

“Tunamwamini Huub Stevens na Mike Buskens kufanya hivyo. Tunamshukuru Manuel Baum kwa juhudi zake bila kuchoka na tunamtakia kila la kheri kwa maisha yake ya baadaye ya kibinafsi na kitaaluma.”


BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!

INGIA MCHEZONI!

13 Komentara

    Watu wanataka ushindi hawataki mambo ya kuwaletea miziro

    Jibu

    Duh noma

    Jibu

    Hii ishakuwa noma sasa

    Jibu

    Shalke wangempa muda

    Jibu

    Sio poa wangempa mda kwanza

    Jibu

    Duh noma

    Jibu

    Aende amwachie nafasi wengine wajaribu

    Jibu

    Dhuu atalii

    Jibu

    Dah

    Jibu

    Hatar sasa

    Jibu

    Aaaaah mbona hivyooo

    Jibu

    Kweli noma

    Jibu

    Atari san

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.