Jonas Mkude mpaka kufikia sasa ametoa jasho na damu kuitumikia Simba wangapi walikuja naye saizi wamepoteza dira , wapi Hassan Isihaka ? Wapi Edward Christopher ? Wapi William Lucian Gallas ? na wengine hakika mkude usiondoke kimya kimya kama Ronaldo . Muda mwingine tusiwe tunajitoa ufahamu kila siku Simba inachukua mafundi ndani na nje ya nchi lakini Jonas hajawahi poteza namba , kuondoka sio dhambi ila usemage mapema tukuage kwa heshima kama alivyoagwa Fransisco Totti , kaka Mkude hiyo siku uje na familia yako maana bila wao usingefika hapo , kaka tunahaidi ukisema mapema tutaandaa wimbo wa kukuaga tutaimba kwa pamoja.

Kaka Mkude mpira ni mchezo unaokusanya watu wa kila aina na kila rika wale kina dada wanaishangiliaga Simba kwa mikogo hawatajisikia vizuri kama hutaagwa mzee , kila nikiangalia namna Andres Iniesta alivyokua anaagwa najiuliza kwanini kwako tushindwe ? , jinsi Xavi alivyoagwa Barcelona dah unaweza tokwa na machozi sasa kwanini kwa kijana wetu tushindwe ? . Pale Stadio Olympico siku Fransisco Totti anaagwa uwanja uligubikwa na machozi kila mtu alilia jamaa kustaafu , kaka we tuambie tu ili tuwaonyeshe watu thamani ya kuitumikia timu yako kwa moyo wako wote , hakika tutaujaza uwanja zaidi ya ile mechi ya Ac Vita.
Siku John Terry anaaga pale Stamford Bridge yalijaa mabango makubwa yakionyesha mchango wa JT kaka usihame kwa surprise kaka , yakumbuke maneno machache ya Iniesta “ Katika mkutano huu na waandishi wa habari nataka kusema huu msimu ni wa mwisho ” chumba chote kiligubwiga na machozi , kila mchezaji wa Barcelona alilia kwa uchungu yule Messi ndio ana roho nyepesi hata kwenye mkutano hakuwepo we tuambie kaka usihofu . Kaka tutakuimbia wimbo wa we are heroes tonight sababu wewe ni shujaa wetu , itakua ni makosa duniani na mbinguni kama hatutakuaga kaka sasa jasho na damu ulivyomwaga vitakosa maana kabisa kaka.
Gigi Buffon aliuliza uwanja mzima wa Allianz Stadium kina dada warembo wa Kitaliano waligubwika na machozi hakika ni furaha isiwe na kifani , Allianz Arena ililoa machozi siku Oliver Khan anaagwa sasa kwa nini kwako tushindwe kaka ? , Mkude embu tuambie tuwaoneshe dunia kwamba Tanzania ni nchi ya aina gani na watamani kuja kucheza . Kaka uongeage na Simba waandae utaratibu maalumu wa kukuaga kaka , zitengenezwe jezi maalumu zenye namba 20 pia zitengenezwe skafu zenye jina lako bila kusahau vitambaa na mapambo mengine mengi , lazima tukuage kaka unastahili kuagwa kaka umefanya makubwa mengi .

Jonas Mkude“ Tokea nikiwa kijana mdogo ilikua ni ndoto yangu kuichezea klabu hii kubwa Tanzania Afrika na dunia kwa ujumla , ahsanteni nyote mliokua nami katika safari hii ngumu ya kutimiza ndoto zangu hakika sitasahau siku zote nitawakumbuka , katika ubaya na uzuri wangu hamjawahi kua tofauti na mimi mungu azidi kuwabariki . Popote pale nitakapokwenda ntaitangaza Simba ”
Hisia zote za mashabiki wa Simba , mashabiki wasio wa Simba na wapenda mpira wote nchini zitakua juu yako hakika , kila mitaa na maeneo yote utakayopita utasikia maneno mazuri saana , watu watakushukuru na kulilia.
makala hii imeandaliwa na EZEKIA JOHN KANDONGA.


Hope mwaikuka
Eeh Afanye hvyo tu
Povel
Thnks meridian bet kwa update za michezo na burudani
Ester jackson
Mmmh kwani mkude anataka kuondoka
Gabriel
Wanogopa Kama kilichowatokea Yanga kwa Morris
Lydia Emmanuel Magoti
Mmmm apana maneno yawatu mkude kuondoka Simba hapana labda aseme nimeichoka Simba sio kwavishawishi vyawatu mkude nasimba Moto wakuotea mbali
David Pere
No kweli kabisa apewe heshima yake maana amewafanyia mengi Wana msimbazi
Theonestina
Kweli kabisa mkude akitaka kustaafu atuambie mapema wapenz wa Simba tumuage kwa heshima
Rehema
Asante sn meridianbet
Theckla
Ni kweli Mana amefanya Mambo makubwa
Shafii
Mkude yuko vizuri na anastahiri kupewa heshima yake clubuni hapo
isha
Mkude unaenda wapi jamani
Elika
Daima mkude ni simba damu hivyo basi hana sababu yoyote ya yeye kutaka kuondoka
Samiah
Jmn jembe langu mkude linaenda wp
Magdalena
Mkude anajua nn anafanya na ndo maana mpaka Leo yupo SimbaSC
Omary lukumbi
Ni heshima kubwa sana kama mchezaj uliechezea club fulan alafu ukataka kuondoka au kustaafu wakakuaga kwa heshima ina taswira kua walitambua mchango wako mkubwa uliotumikia club kwa kipindi chote cha maisha yako
Mwanaidi
Mkude aende wapi tena?
Hilda
Wamwache aende tuu
Tahiya
Izi habari mbna ni zakushtua ivyo Jonas unatak kwenda wapi kijana??
Adelta
Ni vizuri amefanya mambo makubwa sana
Khadija
Namkubali sana mkude#meridianbettz
Neema hassan
Asante kwa makala
warda
Mbona sielewi kwani Mkude anataka kusepa AU Ni ushauri tu#Meridianbettz
Emmy cleopa
Ahsante kwa taarifa
Devotha
Asante kwa taarifa
felister
asiondoke yeye Nani walikuwepo wangapi kwani yeye ndo wakwanza kuichezea Simba…?
Caroline
Simba Wana mbwembwe
lombo
jambo zuri
Salma
Wanaogopa kama kilichowatokea yanga
Hamidu
Kiungo bora Tanzania hakuna kama mkude
Dorophina
Ni vizuri kumpa heshima yake anayostahili
Ernest
Makala nzuri sana, Umegusa kunapo maana imefika wakati kutambua mchango wa wachezaji wetu pindi wanapotaka kustafu au kuhama timu, Salute kwa Mkude
Genia Sikaluzwe
Duuuuh mkude anaenda wapi tena jamani
Sadick
Jonas Mkude namukumbuka kwa faulo aliyomufanyia Morrison na Morrison kupiga na kufunga. Hata hivyo amejitahidi sana kuonyesha kiwango kwa muda mrefu#meridianbettz
Sabrina
Maoni:Mkude mefanya mengi simba ameonyesha kiwango chake
Furahav
Itakuwa poa.
Zeiyana
Namkubali sana mkude anastahili kuagwa kwa heshima msimbazi
Issa
Ndio maana ake