Paulo Dybala Avunja Ukimya.

Kuelekea dirisha dogo la usajili mapema mwezi Januari, maneno mengi yameanza kusemwa. Paulo Dybala na Paul Pogba ni miongoni mwa majina yanayotajwa sana kwa sasa.

Kuna taarifa zilisambaa kwa muda kuwa Juventus wapotayari kubadilishana wachezaji na Manchester United. Walingwa hapa wakiwa ni Paulo Dybala na Paul Pogba, moja kwenda Old Trafford mwingine kwenda Turin.

Baada ya wakala wa Pogba – Mino Raiola kuchafua hali ya hewa kwa maneno makali akiwalengea United, na wakala wa Dybala kuonekana Turin wakati huu ambao mkataba wa mchezaji huyo unamalizka mwishoni mwa msimu ujao (maongezi ya mkataba mpya halisogezwa mbele kutokana na kiwango cha mchezaji kushuka) – wananzengo waliunganisha matukio na kusambaza habari kwamba huenda mambo yameshawiva!!!!!!

Paul Pogba

Waswahili husema “lisemwalo lipo au laja”. Pogba alitumia ukurasa wake wa Instagram kusisitiza kuwa yeye ni Man United na itaendelea kuwa hivo, Dybala na yeye ametoa tamko lake kuhusu hili.

“Vitu vingi ambavyo sio vya kweli vinasemwa vikihusisha mkataba wangu. Wakala wangu alikuwa Turin kwa muda mrefu na wala hakuitwa na klabu. Inaniumiza kusikia maneno yanayohusisha uwekezaji.

“Itakuwa ni jambo jema kama ukweli utasemwa, kwasababu kuongelea hivyo vitu kwa wakati kama huu ni kunichonganisha na mashabiki kwa mapenzi makubwa niliyonayo kwa Juventus.” Paulo Dybala aliiambia Sky Italia.


BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!

INGIA MCHEZONI!

18 Komentara

    Amefanya vizuri

    Jibu

    Vizuri ngoja tuone kwenye dirisha dogo naniataenda wapi yupi atabaki wapi ngoja tuone

    Jibu

    Jambo alilolifanya ni jema tunasubilia tu majibu

    Jibu

    Ni jambo nzuri san

    Jibu

    Safi sana alichokifanya

    Jibu

    Mbona wanatuchanganya jamani bora huyo paulo alivyovunja ukimiya

    Jibu

    Ni jambo zuri

    Jibu

    Pogba akomae asiende klabu nyingine abaki hapo hapo

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Good

    Jibu

    Good

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Anatisha uwanjan

    Jibu

    Inapendeza

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Safi

    Jibu

Acha ujumbe