Ronaldo Wasiwasi Kuwakosa West Ham

Mshambuliaji wa timu ya Manchester United Cristiano Ronaldo anawasiwasi wa kuukosa mchezo dhidi ya West Ham kutokana na matatizo ya shingo.

Ronaldo alikosa michezo miwili kwa tatizo la misuli na alirejea kwenye mchezo wa siku ya jumatano dhidi ya  Brentford na Man Utd kushinda kwa 3-1, kulitokea sintofahamu baada ya kutolewa nje huku mreno huyo akionekana kutoridhika.

Ronaldo
Cristiano Ronaldo

Kocha wa muda Ralf Rangnick alielezea hilo kwenye kituo cha klabu hiyo MUTV, “Cristiano ni swali ambalo bado tunajiuliza kwa sababu ana matatizo ya shingo, alianza mataibabu jana kwa masaa mawilli au matatu, kwaiyo tutaangalia hali yake kwa siku ya leo.

“Edinson Cavani bado hajaanza mazoezi na timu na tunatarajia kusimamisha mazoezi leo na tutaangalia jinsi ya kufanya maamuzi ya mwisho baada ya kumaliza mazoezi leo, kama atakuwepo kwenye mchezo wakesho.”


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe