Rafael Nadal kwa anafikilia zaidi kushinda taji la Australian Open ili aweze kuwa mchezaji namba moja mwenye Grand slam 21 na kuwapita Novak Djokovic na Roger Federer kwenye listi ya wachezaji wenye mataji mengi zaidi kwa muda wote.
Kesho siku ya ijumaa Nadal anatarajia kucheza mchezo wake wa nusu fainali na Barrettini, huu ndio mtihani wake wa kwanza ambao uatabidi aupitie ili aweze kutimiza azma yake katika michuano ya Australian Open
Rafael Nadal hajashinda taji la Australian Open tokea mwaka 2009, kwa sasa hii ndio nafasi yake adhimu ya kuweza kushinda taji hilo kwani kutokuwepo kwa Djokovic na Federer kunampa nafasi kubwa ya kuweza kunyakuwa taji hilo.
Djokovic alitolewa kwenye mshindano hayo baada ya kutokizi masharti ya kuingia nchini Australia kutokana na kanuni za chanjo ya Uviko-19, wakati Federer bado anauguza majeraha yake ya goti na anatarajia kuwa nje zaidi kwa miezi kadhaa.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.