Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Borussia Dortmund wanafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa na Manchester United Anthony Martial, 25, ikiwa mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, 21, ataondoka katika klabu hiyo msimu wa joto.

Barcelona na Real Madrid watakua miongoni mwa klabu zinazomwania kiungo wa kati wa Leicester Youri Tielemans, 24, ikiwa kiungo huyo wa kati wa Ubelgiji atauzwa, msimu ujao.

West Ham wanashughulikia mpango wa kumsajili kiungo wa Juventus Weston McKennie, 23, na mazungumzo tayari yamefanyika juu ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Marekani.

 

McKennie

Tetesi zinasema, Winga wa zamani wa Bournemouth Arnaut Danjuma, 24, anafuatiliwa kwa karibu na Liverpool baada ya Mholanzi huyo kuanza msimu vizuri katika klabu yake mpya ya Villarreal.

Tetesi zinasema, Liverpool wamekuwa wakimfuatilia kiungo wa kati wa Porto Mcolombia Luis Diaz, 24.

Tetetesi zinasema, Chelsea na Liverpool zinamnyatia winga wa Newcastle na Ufaransa Allan Saint-Maximin, 24.

 

Tottenham huenda wakasubiri hadi msimu ujao badala ya Januari kabla ya kujaribu kumuuza tena Dele Alli,25, ikizingatiwa thamani ya kiungo huyo wa kati wa England ilivyoshuka.

Tetesi zinasema, Barcelona wamepokea ofa kutoka kwa kampuni ya Dubai ya kununua deni la klabu hiyo la euro bilioni 1.5 (£1.2bn).

Tetesi zinasema, Barcelona wameungana na Bayern Munich katika kinyang’anyiro cha kumsaka winga wa Ajax Mbrazili Antony, 21.

 

Flick Anataka Mengi Zaidi Kutoka Sane.

Chelsea na Bayern Munich kwa sasa hawana mpango wowote wa kubadilishana wachezaji kati ya winga wa Marekani Christian Pulisic, 23, na winga wa Bayern Mjerumani Leroy Sane,25, licha ya uvumi unaoendelea.

Kocha wa Roma Jose Mourinho anataka kumleta kiungo wa kati wa Tottenham na Ufaransa Tanguy Ndombele, 24, katika klabu hiyo.

Tetesi zinasema, klabu ya Real Betis wameanza mazungumzo ya kurefusha mkataba wa mshambuliaji wa Ufaransa Nabil Fekir, 28.

Real Madrid wanamtaka kiungo wa Inter Milan Alessandro Bastoni, ijapokuwa thamani ya sasa mlinzi huyo wa Italia mwenye miaka 22, inakadiriwa kuwa euro milioni 60 (£51.7m).


SPACE SPIN NA MERIDIANBET.

Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe