Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Everton na meneja Rafael Benitez wamekubali kuachana, huku mazungumzo yakiendelea kuhusu taarifa za kuondoka kwake. Duncan Ferguson ameombwa kuchukua nafasi ya meneja wa muda.

Kiungo wa kati wa Leeds United wa Uingereza Kalvin Phillips anasakwa na Liverpool, lakini Leeds wako tayari kumwacha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kwenda nje ya nchi, huku Paris St-Germain, Bayern Munich na Real Madrid wakiwa miongoni mwa wawaniaji wake.

Chelsea lazima waongeze ofa yao ya pauni milioni 33 ikiwa wanataka kumsajili Frenkie de Jong wa Barcelona. Barca wanataka euro milioni 60 (£50m) kwa kiungo huyo wa kati wa Uholanzi, 24, ambaye pia anasakwa na Bayern Munich.

 

Frenkie De Jong Xavi

Mkufunzi wa muda Ralf Rangnick hajafurahishwa na kitendo cha Manchester United kusita kumuunga mkono kwenye dirisha la usajili na ana wasiwasi kuhusu ushawishi mkubwa atakaokuwa nao atakapoanza kazi yake ya ushauri kwa miaka miwili msimu wa joto.

Kocha wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino amekuwa akihusishwa na kuchukua nafasi ya meneja wa Manchester United lakini, bila mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili, klabu nyingine kubwa ya Ulaya pia inavutiwa na huduma ya Muargentina huyo.

Mshambuliaji wa Misri, Mohamed Salah anakataa kuyumbishwa na imani kwamba ana thamani ya pauni 400,000 kwa wiki kusaini mkataba mpya na Liverpool. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 utakamilika msimu wa joto wa 2023.

Tetesi zinasema, Arsenal wamefanya mazungumzo yasiyo rasmi na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Diego Costa, 33, Anatarajia kuondoka Uhispania mwezi huu.

 

Newcastle United wanatarajiwa kuanza tena mazungumzo na Sevilla wiki ijayo kuhusu kumsajili beki wa kati wa Brazil Diego Carlos, 28.

Tetesi zinasema, Newcastle imekuwa na ofa ya zaidi ya euro milioni 40 (£33.4m) kumnunua beki Mfaransa mwenye umri wa miaka 20 Benoit Badiashile iliyokataliwa na Monaco.

West Ham wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Newcastle kwa ajili ya kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United Muingereza Jesse Lingard, ambaye mkataba wake utamalizika msimu wa joto.

Tetesi zinasema, Barcelona wana nia ya kumsajili Roberto Firmino kutoka Liverpool, ambaye anataka euro milioni 20 (£16.7m) kwa mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 30.

 

Roberto Firmino

Mshambulizi wa Inter Milan na Croatia Ivan Perisic, 32, anavutiwa na Chelsea, huku mkufunzi Thomas Tuchel akitaka kusajili beki wa kushoto kufuatia jeraha la mlinzi wa Uingereza Ben Chilwell, 25.

Tetesi zinasema, Atletico Madrid hawana nia ya kumuuza mshambuliaji wa Ureno Joao Felix mwenye umri wa miaka 22 mwezi Januari au msimu wa joto.

Aston Villa wanafikiria kumnunua mlinda mlango wa Coventry City Muingereza Simon Moore, 31. Meneja wa Villa Steven Gerrard anataka kuongeza ulinzi kwa mlinda mlango wa Argentina Emiliano Martinez, 29.

 


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe