Trent anakuja kutupa somo jipya namna mpya na darasa jipya , anakuja kutupa vitu ambavyo hatukuviona kwa muda kidogo beki wa kulia mwenye takwimu nyingi za hatari za kushambulia kuliko kukaba . Wapo wanaosema kijana anasweet zaidi akicheza kama kiungo lakini Klopp bado hajaamua iwe ivyo , kuna waliomshuhudia Dani Alves pia wapo waliomfaidi Phillip Lam , unaweza changanya utamu wao ukampata Trent.
Soka la kiingereza lilikua na ustaarabu wake kabla ya kuja Arsene Wenger na pasi zake nyingi , mara nyingi build up ya magoli ilianzia pembezoni mwa uwanja , watakuja kupitia pembeni na kupiga mashuti au watapiga krosi nyingi . Arsene Wenger alikuja na utamaduni wake kwanza lazima timu imiliki mpira ndipo wamfuate mpizani kwa hatua lakini aliposhindwa kujiongeza ukawa mwisho wake , kwa sasa hata Guardiola ameamua kuwaiga wazawa magoli yake mengi yanatokea pembeni kuliko katikati .

Pengine Dani Alves anaweza kua moja ya mabeki wa pembeni wa kulia bora kabisa kuwahi kutokea , jamaa aliweza kila aina mchezo kuanzia pasi fupi fupi pia anazijua one-two vizuri anapiga krosi za uhakika pia ni fundi wa mipira iliyokufa , kuna Phillip Lam naye anaingia humo hata Cafu anajaa humo kiuhakika . Wote hawa walitupa aina tofauti ya mlinzi wa kulia hadi kila mtu akasema yake , lakini Jurgen Klopp amekuja na aina yake ya kipekee , kifupi wote hao Alves na Lam wanajua kuchezesha timu ila Trent ni darasa jipya.
Andrew Pirlo aliitwa Deep Lying Playmaker huyu alikua kiungo mshambuliaji lakini alianzia harakati zake nyuma kabisa , tukumbuke tu Pirlo alikua kiungo ina maana hizo harakati alizifanyia akiwa kama kiungo . Baada ya kumtathmini sana Trent leo nimeliona jina jipya sehemu na anaitwa DEEP LYING WIDE PLAYMAKER , ndio inabidi aitwe ivyo hakuna namna kijana anakosa sifa za kiulinzi ila anasifa za kwenda mbele zaidii , Trent mpe pasi hata akiwa eneo lake la hatari atafanya jambo zuri tu ila mwambie akabe ndani ya eneo la hatari utampa lawama za bure.

Ujio wa kiungo fundi mkabaji wa Kibrazil Fabinho Travarez ndio ulimfungulia Trent dunia kua anachotaka , iko ivi ili unyonye uwezo woote wa Trent lazima pawe na mtu anakaeziba nafasi yake wakati yeye ameenda kufanya anachotaka . Alikuwepo Emre Can huyu jamaa alikua kiungo mzuri sanaa na alikua mkabaji lakini alipenda sana kushambulia alafu alikua homa za vipindi , Jordan Handerso hakuonekana kuwasoma wapinzani kiulinzi hata kushambulia hakuwasoma lakini ni nahodha . Pengine Trent na Robbo ndio vijana hatari sana kwa sasa lakini hatuangalii kina nani wanawapa hua uhatari , uwepo wa fabinho pale Liverpool ndio unaleta usawa sana na timu kupata balance.
Trent anakupa vitu vingi sana mpaka raha kwanza ni fundi sanaa wa kupiga pasi ndefu kiustadi yeye kuhamisha uwanja ni kama kunywa maji , ukimmark sana basi anaanza kupia one-two sababu yupo huru sana na mpira , trent ni mjuzi wa kukimbia kuziwahi pasi iwe kwa kuingia ndani ( underlap ) au pembezoni mwa touchline ( overlap ) , kuna muda anaungana na viungo kama pembeni kumebana sana , anapiga mipira iliyokufa kwa umahiri wa hali ya juu , anatengeneza nafasi za kufunga kwa umahiri mkubwa pia ana mguu mzuri wa kufunga.


mwakalosi
klopp hapa alilamba dume na kumaliza mchezo
Theckla
Ni beki mzuri Sana
Gabriel
Trent yuko vzur sana na sifa ya kupiga pasi ndefu ndo usiseme fundi sana huyu jamaa
Rehema
Uko vzr ni kocha mzr
Povel
Trent Arnold yupo vzr sana kwny kushambulia Ila kwny kukaba ndo tatizo thnks meridian bet kwa gud news
dorophina
Mchezaji mzuri sana
Furahav
Hatari sana Anord.
Emmy cleopa
Beki yuko vizur sana
David pere
Dogo anajua Sana kutimiza majukumu yake akiwa uwanjani
Salma
Yupo vizuri
Mariam mtandama
Mzur
Adelta
Yup vizuri sana
Elika
Asanten kwa taarifa meridianbet
Amani
anatengeneza nafasi za kufunga kwa umahiri mkubwa pia ana mguu mzuri wa kufunga.#meridianbettz
Tatu
Trent yupo vizuri
mathayo sonje
klop alipata beki mshambuliaji, ambaye anakila kitu awapo uwanjani, kila mmoja anamuonaga Anord awapo kiwanjani hatanii kazikazi tu. #meridianbet
Tahiya
Yuko vizur
Agness
Yuko vizuri
Devotha
Ni beki mzuri sana
Lombo
kisik
Mwajuma
Nibeki anaejielewa nin anafanya
Magdalena
Dogo yupo vizuri Sana anajua jinsi gani ya kujitengenezea nafasi ya kufunga magoli
Mwanaidi
Safi sana
Theonestina
Namkubar Sana uyo jamaa
Juliana
Beki mkali
Lydia Emmanuel Magoti
Yupo vizuri sana
Antony Luseno
Mfumo wao wa uchezaji uwa unasaidia kuipa timu matokeo
Hope mwaikuka
Ni beki poa sana
Rehema Dickson
Bonge moja la beki
Khadija
ni beki nzuli#meridianbettz
Samiah
Yupo vizuri sanaaa
Hamidu
A.A.. mkali wa assist pale EPl .! Dogo mnamkubali Sana# meridianbettz
aisha
Ni beki hatari
Asha
Thnks meridian bet tz kwa gud news
Swai
Nibek mzuri sana
frank patrick
Klopp amchezeshe midle dogo kama Stevie G
Adelta
Anord Ni miongoni mwa wanaoleta mafanikio ya liverpool
felister
anajua nini anachofanya
Isaya massawe
Anajitahidi sana huyu beki na anafanya vizuri
Neema hassan
Beki mzuri sana
Ester mmakasa
Ni makala nzuri sana kwa watanzania wote wenye malengo na wenye vipaji kama hawa walioandikwa makalani ,tujifunze na tufanyie kazi .
winfrida
liver wanajivunia kuwa na beki bora
Carolyne
Ni beki makini uyu
SADICK
Mchezaji mzuri lakini hafai kuwa beki #Meridianbettz
Hidaya Mohammed
Anajua nini anachokifanya
Ernest
Trent ataweka record kubwa sana kwenye ulimwengu wa soka endapo tu ataendelea kukaza Buti.
Shafii
Ni beki bora timu ikiwa inashambulia
Mwanahamisi
Safi sana
Warda
Club ya Simba ilikuwa inamtaka huyu #Meridianbettz
Evaluziga
Beki mkali sana
Ester
Yuko vizuri
Kenani
Yuko poa sana
Neema juma
Bekii makinii sana
Genia skaluzwe
Beki Yuko poa sana
Asia Abdy
Trent fundii
Issa
Arnold ni mahiri na beki mpambanaji
farida ahmadi
Trent yupo vzr Sana ni beki bora hajawahi kuiangusha timu yake Safi Sana hongera klopp kwa kupata beki mzuri