Maisha hayana adabu , maisha yanaweza kukupeleka sehemu ambayo hukuwahi waza kuwepo na yakiamua yameamua . Masikini kipindi mtu anasoma anawaza kua mwanasheria lakini mwisho wa siku anakua mwalimu wa Kiswahili sekondari , ana ndoto za kua rubani wa ndege mwisho wa siku anakua muuza duka , dada zetu wanaodanga hawakuwahi waza kufanya hiyo kazi wameikuta ukubwani . Maisha ndivyo yalivyo hayana adabu na hayako fair , yanakufanya uwe kwenye hali ambayo hukuwaza kua.

Mambo yanavyozidi kua mazuri ndipo matarajio hua mengi zaidii , unajikuta tu unajiwekea malengo makubwa kama vile mtoto wa shule jinsi inavyozidi kufaulu ndipo anawaza kazi za udaktari na urubani . Nyota inavyozidi kuwaka sanaa hata watu wanaokuzunguka wanakua namatarajio makubwa na wewe , baada ya Mbwana Samatta kusajiliwa TP MAZEMBE watanzania walikua na matarajio makubwa na Mbwana Samatta achana na wale waliomjua toka Mbagala Market ,safari ya kwenda kwenda KRC GENK na Aston Villa watu walitarajia na walijua itatokea atafikia hiyo hatua . Barcelona walikua na matarajio na Messi ndio maana wakaamua kumlea.
Shiza Ramadhani Kichuya yupo katika kanuni ya maisha yameamua kumpeleka asipo tarajia , nani alitarajia wakati kama huu hatakua chaguo la kwanza ? wala pili pengine hata la tatu hasiwepo ? Nyakati zinakwenda kasi sanaa tena zipo kasi sanaa watu wameshasahau ile kona ya moja kwa moja dhidi ya Yanga “kichuya kona”, Kichuya alikua Almasi tangu pale Manungu watu walimpenda na walimuogopa , kila kocha aliyekwenda kucheza na Mtibwa lazima awaze namna ya kumzuia Kichuya kuanzia winga ya kulia hadi kiungo mshambuliaji alikua zaidii ya Almasi , ulikua huwezi kupanga first eleven katika timu zote kubwa hapa bongo bila kumpanga Kichuya…..
Shiza ilikua lazima akacheze soka la viwango vingine, mabalaa yake wengi walitarajia akafayanye TP MAZEMBE , AL AHLY , MAMELODI SUNDOWN au sehemu yoyote kubwa Afrika na Ulaya , kipindi yupo kwenye ubora wake kwanini hakuondoka hakua na timing nzuri na ubora wake . Badala ya kuondoka wakati akiwa bora aliondoka baada ya kuonekana hana nafasi , kanuni ya maisha ilichukua nafasi yaliamua kumuondoa wakati asioutarajia na kuua matarajio ya wengi . Kanuni si lazima ifuatwe zingine lazima zipingwe, wengi wanafeli sanaa katika maisha kisa wanafata sanaa sheria sio kila sheria inakupa muongozo mzuri pengine sio kila ndoto lazima itimiee


mwakalosi
huyu alijisahau kabisa kama yeye mchezaji ananenepa nenepa hovyo
Theckla
Kichuya alikuwa ni mchezaji mzuri ,tatizo la wachezaji wakitanzia wanalewa sifa mapema mwisho ubora wao unapotea kabisa
Ester mmakasa
Duuh!yuko katika wakati mgumu kichuya ,inabidi apambane na aongeze juhudi kama zamani atarudi katika nafasi yake.
Gabriel
Hamna bhana kichuya fundi ila akapanda middle mzur wa kutengeneza na hilo ndo udhaifi wa Simba mkubwa sana
Rehema
Kichuya Yuko vzr sema tu kajisahau Kama yy ni mchezaji mazoezi kayatupa
Povel
Kichuya wakala wake alimwangusha sana kwa kiwango chake akustail kucheZ timu za madaraja ya chn Kama vle thnks meridian bet kwa update
Lombo
habari mazur
Mariam mtandama
Habari mjema
Furahav
Daaa!!! Kweli maisha ni safari ndefu sana.
mathayo sonje
Kila wakati unakua na kanuni yake, hapa ukikosea kuifuata basi lazima baadae mambo yawe ndivosivyo, kichuya alisahau kama muda unaenda na mambo yanabadilika, hayo ndio matokeo yake
Devotha
Wakati wake ulishaisha
Tahiya
Maisha yana mambo mengi sana kichuya alitamba kwa wakati wake sasa awaachie wenzie
Salma
Alijasahau sana
Emmy cleopa
Habar njema
Magdalena
Kichuya namkubali Sana yupo vizuri
David pere
Bado kiwango anacho Ila tatizo hapa bongo misumari mingi sana
Amani
Jambo zuri
Antony Luseno
Ulevi wa sifa ndo ulimpotosha
Mwanaidi
Ni vyema kuamua hivyo
Hope mwaikuka
Kuanza upya sio ujinga
Theonestina
Jamani nampenda Sana kichuya.arudi kuwa bize na mazoezi.ili arudi kwenye ubora wake
Juliana
Da! Kichuya namkubali sana
Rehema Dickson
Kichuya yuko vizuri ila alilewa sifa akajisahau ndo tatizo la wachezaji wa bongo ilo
Mwajuma
Kichuya anajipya kwa sasa
aisha
Duuh kichuya anatakiwa afanye mazoezi sana
Samiah
Nihabari njema sanaaa
Khadija
Daah kichuya yupo vizuli sana#meridianbettz
Lydia Emmanuel Magoti
Kichuya nimchezaji mzuri Sana namwenyekasi yampira kwasasa azidi kuongeza Juudi aludi kwenye mwelekeo wake wakisoka
Hamidu
Kichuya amefeli kurudi bongo..nilitegemea angekwenda hata south Africa#meridianbet
David pere
Ni vizuri kuanza upya sio ujinga
Asha
Ni mchezaj mzur Sana thnks meridian bet tz
dorophina
Kichuya yupo vizuri sana kwenye mpira
Elika
Popote kambi kichuya
frank patrick
Dah kweli bongo Nyoso
Swai
Duuu tatzo kulewa sifa ndio kunakowapotezaa
Agness
Yuko vizuri namkubali sana
felister
kila kitu kina wakati wake kichuya muda wake umeshaisha
Isaya massawe
Hii imekaa vizuri ni somo kwa upande fulani
Neema hassan
Kichuya yuko vizuri sana
winfrida
afanye mazoezi sana kichuya asipoteze ndoto yake
Carolyne
Yote ni maisha
SADICK
Dah bonge la makala. Pole yake#Meridianbettz
Adelta
Kichuya Yuko vizuri
Ila kwa sasa afanye mazoezi kwa wingi
Hidaya Mohammed
Ameshapoteza brand yake
Shafii
Uwezo ushaishia hapo
Ernest
Kweli Kichuya anaonekana anastress na Maisha yake ya soka, Asante Meridianbet kwa makala nzuri.
Warda
Kweli maisha hayana Adabu
Mwanahamisi
Habari njema
Evaluziga
Ni habari njema
Ester
Aliaza vizuri baada ya kujulikana sasa amekuwa hana ubora abadilike kuwa maarufu katika soka isiwe shida pambana uwe juu na sio kujiachia
Kenani
Itakua poa sana
Neema juma
Kwa kwelii nimejifunza kitu hapa. Na pia sio kila ndoto lazima itimie
Genia Sikaluzwe
Kichuya na mkubali Sana kwenye mpira
Zeiyana
Kira kitu kinaenda na bahati mungu ndiye hanapanga..!bado sana kichuya mri hunaruusu wew pambana tu