Katika ligi kuu ulimwenguni zilizofaidi utamu wa wachezaji wa kidachi ,ligi ya Uingereza ni mojawapo.Achana na kina Virgil Van Dijk wa majogoo wa Liverpool na wengineo wa sasa .Walikiwepo kina Jaap Stam,Rud Van Nestoroy.
Katika orodha hiyo unamsahau vipi aliyekua golikipa wa Manchester United ,Edwin Van de Sir aliyepiga clean sheets 14 katika msimu wa 2008/2009 .Ndiye Golikipa pekee raia wa Uholanzi anayemiliki cleen sheets kuwahi kucheza ligi kuu ya Uingereza akiwa na jumla ya clean sheets 132.

Alikuwepo bwana mashoto Robin Van Parsie,Marc Ovamarc ,Mimacho Jimmy Floyd Asselbaink.Kabla ya hapo Walikuwepo pia kina Hans Segers na Michel Volnk na kutengeneza idadi ya wachezaji zaidi ya 133 wa kidachi mpaka sasa waliocheza ligi hiyo ya Malkia Elizabeth
Mechi 38 za ligi mkashinda 26 na kutoa sare mechi 12 ni vitu ambavyo hutokea Mara moja baada ya miaka mingi katika ulimwengu wa soka.
Perp Gardiola atakua amenielewa sana hapa.Msimu wa 2017/2018 alipojaribu kufanya kama mlivyofanya aliishia kuvunja rekodi ya kua na alama nyingi lakini sio kucheza ligi pasipo kupoteza mchezo hata mmoja.Majogoo wa Liverpool msimu huu walikipata walichokipata walipojaribu kuwaiga.

Ulimfanya mfaransa Thiery Henry afurahie kucheza na kufunga kadri anavyojisikia.Wewe na bwana Matekenya Robert Pires mliufanya mpira wa miguu uonekane ni kitu rahisi kuliko kumeza mate
Kaka Denis Bergkamp,nafahamu kama haukuwahi kuchukua ufungaji bora kwenye ligi ya Uingereza kama walivyofanya wadachi wenzako kina Jimmy Floyd Hasselbaink, Robin Van Persie na Van Nestoroy lakini ligi ya Uingereza pamoja na washika bunduki wa kaskazini mwa London hawana wanachokudai.
Wataanzaje kukudai ikiwa katika mechi 315 ulizocheza pale Highbury umefunga magoli 87 na kutengeneza 94?.Wakudai nini kama Asernal ya Wenger kupitia miguu yako umeicha na vikombe vitatu vya ligi kuu katika misimu ya 1997/1998,2001/2002/2003/2004?.
Hawakudai chochote wakikumbuka mara nne umekuwa mchezaji Bora wa mwezi katika ligi pendwa Ulimwenguni.Ulifanya hivyo August 1997,ukarudia September 1997 ,Kama haitoshi March 2002 ukamalizia February 2004.
Bergkamp ,Bergakamp Jina la kijanja sana kimaana kule Ujerumani kabla ya ujio wa Adolf Hitler . Maana yake ni mtoto wa mjini.Wakati pale Sweeden ukisema Bergkamp utakua ukimaanisha mapambano ya milimani.


mwakalosi
fundi wa kidachi master assist
Ibrahim
Uyo ni mtu hatari
Theckla
Alikuwa fundi wa mpira na kihalisia alikuwa ni mtu wa kujituma uwanjani
Gabriel
Jamaa tunamkumbuka sana kipindi hicho arsenal iko moto
Rehema
Namkubali sn anajua mpira
Povel
Thnks meridian bet kwa update
Lombo
Bergkemp n mchezaj yuko vzur
Emmy cleopa
Ahsante meridian kwa habari nzuri
Furahav
Mchezaji hatari.
Mariam mtandama
Mchezaji mashuhuri sana
Salma
Fundi wao
Amani
likuwa fundi wa mpira na kihalisia#meridianbettz
Adelta
Alikuwa fundi mzuri wa mpira
Tahiya
Mchezaji mzuri
Agness
Huyo ni mchezaji mzuri
mathayo sonje
wenga hapa alilamba dume maana mambo aliyoyafanya pale si yakitoto, wana Arsenal wananielewa nikimtaja BERGKAMP!!!
Devotha
Asante meridianbettz kwa taarifa
Mwajuma
Huyu jamaa aliifanya Arsenal ikawa moto
David pere
Alifanya vitu ambavyo mpaka Sasa hakuna mchezaji yoyote pale Arsenal atavirusia
Mwanaidi
Mchango wake hausahauliki kamwe
Magdalena
Mchango wake katika soka ni mzuri ndo maana hawezi kusahaurika
Antony Luseno
Ni nadra sana kuwapata viungo kama huyo
Theonestina
Asante meridianbet kwa taarifa
Samiah
Nifundi mzuri sana wa mpira
Hope mwaikuka
Mtu m bad
Juliana
Uyo jamaa ni fundi
Lydia Emmanuel Magoti
Mchezaji mzuri Sana huyo fundi mpira
Rehema Dickson
Mmyama umyaman noma sana uyu jamaa
Khadija
Alikuwa fundi wa mpira#meridianbettz
Hamidu
Fundi wa Mpira anayeogopa kupanda ndege ✈️✈️#meridianbettz
aisha
Yuko vizuri
dorophina
Jamaa fundi sana wa mpira
Asha
Thnks gud news
frank patrick
Aliweka mgoal mmoja hv wakihistoria epl mpaka leo ni gumzo
Swai
Alikuwa fundi hatari sana
felister
bargkamp atakumbukwa daima arsenal
Isaya massawe
Alikua was moto hatari
Neema hassan
Ana mchango mkubwa sana katika game#meridianbettz
Carolyne
Bergkamp yupo vizuri
winfrida
mchezaji mzuri sana
SADICK
He was talented footballer#Meridianbettz
Ester mmakasa
Ni kiungo mzuri sana Bergkamp anastahili sifa.
Hidaya Mohammed
Bergkamp kweli ni mapambano ya milimani
Ernest
Mdachi mwenye Mbilinge mbilinge uwanjani
Shafii
Hawezi kusaulika kwa kazi kubwa alio ifanya arsenal
Mwanahamisi
Mchezaji mzuri
Evaluziga
Mchezaji hatari
Ester
Habari zuri sana
Kenani
Fund mweny maufundi yake
Neema juma
Mchezajii mzurii mnoo
Genia Sikaluzwe
Ni fundi mzuri wa mpira
Asia Abdy
Jamaa anajua
Rehema Dickson
fundi wa mpira na kihalisia alikuwa ni mtu wa kujituma uwanjani