WWE: Walioiwakilisha Vyema NXT

HII ni sehemu ya kukusanya nguvu ya pamoja na kuangalia namna ya kujiendesha wenyewe na wakaweza kutengeneza pesa ya aina yake kupitia kundi hilo. Wakati linaingia sokoni hakuna hata mmoja aliyekuwa amependezwa nalo hata ikawa inafika wakati hakuna taji lolote kutokana na kukosa watu wenye uwezo mkubwa wa kupambana na nafasi hiyo.

Ila jambo jema zaidi miaka ya baadaye watu wakaanza kukiona kile ambacho hapo nyuma hakikuwa kikionekana na kuanza kuthamini kazi zao wakiingia ulingoni. Kwa sasa wana majina ya watu ambao kwa hakika wana uwezo mkubwa wa kuleta ushindani ulingoni hata wa kutetea mataji makubwa mbele ya wakongwe kwenye michuano hiyo.

Wafuatao ni baadhi ya nyota wa WWE NXT walioweza kujenga majina na historia ya nidhamu mbele ya michuano mikubwa:

Kevin Owens, kuna mechi ambayo wengi waliwahi kudhani kwamba nyota huyo angezikwa kabisa na John Cena lakini mambo hayakwenda vile wengi walidhani yangetokea. Alionesha upinzani mkubwa na hata sasa mambo kama yale yamemjenga vizuri hadi amekuwa nguzo ndani ya kundi lao. Hadi sasa ni miongoni mwa nyota ambao wanafanya vizuri ndani ya kundi lao hilo.

Becky Lynch, tangu ajiunge na NXT 2015 alionekana kama ni miongoni mwa watu ambao wanafanya vizuri zaidi kwenye ulingo hasa baada ya kushindwa kufikia malengo yao mapema. Baada ya kuingia kwenye SmackDown 2016 aliweza kuonesha kwamba ni chaguo sahihi kabisa.

Alexa Bliss, baada ya kuwa na ukame wa muda mrefu alifanikiwa kutwaa taji kwenye SmackDown ya 2016 kutokana na uwezo wake mkubwa aliokuwa nao mbele ya wapinzani wake aliokutana nao ulingoni. Pamoja na hatua hiyo lakini bado kuna walakini kwenye uwezo wake kutokana na majeraha anayokumbana nayo mara kwa mara kwenye mapigano.

Mbali na hao kuna wengine ambao uwezo wao wakiwa uwanjani bado umekuwa na ukakasi mkubwa baada ya kushindwa kufikia malengo ambayo wao wenyewe pamoja na kampuni yao iliyaweka. Baadhi yao ni Tyler Breeze, Sami Zayn lakini kwa sababu ni kikundi ambacho kina watu wanaowabeba wengine bado hakijaharibika na watafanya kubwa zaidi kurejesha heshima.

3 Komentara

    Walisumbua sana hawa wanawake

    Jibu

    Mmh wakali hawa

    Jibu

    Nawakubali sana.

    Jibu

Acha ujumbe