Mmachinga Aipa Ushindi Yanga

NYOTA wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa Yanga Princess Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ anaimani kuwa Simba watapoteza kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utachezwa leo kwa Mkapa.

Chinga ambaye anashikilia rekodi ya kufunga mabao 26 kwenye msimu mmoja wa ligi alisema, Yanga watafanya vema kwenye mchezo huo kwa sababu kikosi chao hakijabadilika sana na wachezaji wote ambao waliipa mafanikio timu hiyo msimu huo msimu uliopita bado wapo.

Akizungumzia mchezo huo Chinga alisema: “Yanga naona wanakwenda kufanya vizuri kwenye huo mchezo kwa sababu ukitazama timu haijabadilika sana na wachezaji wengi walioipa timu ubingwa bado wapo.

“Hivyo muunganiko huo bado upo kwenye timu na wale wachezaji wapya ambao wameongezeka naona kabisa wanakwenda kuipa faida Yanga ingawa haitakuwa rahisi kama ilivyo kawaida.”

Kesho saa 1 usiku uwanja wa Mkapa utashuhudiwa mchezo huo wa dabi ambao utakuwa ni ishara ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2022-23.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.