Rais CAF Ataja Sababu za Kuanzisha Super League

Raisi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika, Patrice Motsepe ametangaza kuanzishwa kwa mashindano mapya ya vilabu Afrika yatakayo julikana kama “CAF Super League” alipokuwa akizungumza katika mkutano mkuu wa CAF uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha nchini Tanzania.

Motsepe alisema sababu za kuanzisha mashindano hayo ni kuwanufaisha wachezaji wa kiafrika ambao wamekuwa wakipata kipato kidogo ukilinganisha na wale wa Ulaya.

Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi Agosti,2023 ikihusisha timu 24. Malengo makubwa ya michuano hiyo ni kusaidia timu za Afrika kiuchumi ili kuweza kuendana na kasi ya ukuaji wa mchezo wa mpira wa miguu na kuweza kushindana na timu kubwa nje ya Afrika.

Motsepe alisema: “Ukiwa mchezaji wa mpira unakuwa na muda mchache wa kufanya kazi kwahiyo inabidi upate pesa nyingi ili baada ya kustaafu mpira uweze kumudu kutunza familia.

“Kwa Afrika timu hazilipi vizuri ukifananisha na ulaya ndo mana tunashindwa kuwabakisha wachezaji wetu wazuri.

“Kwa kutokuwa na wachezaji wazuri inapelekea ligi zetu kutotazamwa sana hii ikatufanya tuje na wazo la kuanzisha Africa Super League ili kuinua timu zetu kiuchumi na kupata wachezaji wazuri kukuza ligi zetu.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.