Klabu ya Al-Hilal ya Sudani imegoma mechi yao ya mzunguko wa pili wa ligi ya Mabingwa Afrika katika hatua ya awali ya ligi baada ya mchezo wa kwanza kupigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Baada ya mchezo wa kwanza kumalizika jijini Dar-es-salaam kwa sare ya goli moja kwa moja na mchezo wa pili utapigwa katika jiji la Khartoum nchini Sudani katika dimba la Omdurman kati ya Al-Hilal dhidi ya Yanga.
Katika mchezo huo ambao inaelezwa klabu ya hiyo imegomea kiasi cha milioni 200 kutoka kwa kampuni ya kurusha matangazo ya Azam Media na kutohitaji mchezo huo kurushwa mubashara kutoka nchini Sudani.
Hali imewashangaza watu wengi lakini ikumbukwe katika hatua za awali na hatua za kwanza klabu ndio ina haki ya matangazo ya michezo yao hivo shirikisho la mpira barani Afrika halina nafasi na nafasi yao inakuja kuanzia hatua ya makundi.
Mpaka sasa haijafahimika sababu za msingi za klabu ya Al-Hilal kwanini inagomea mchezo huo kurushwa mbashara.

