Miura: Avunja Rekodi Yake Mwenyewe Kama Mchezaji Mkubwa Zaidi Duniani.

Kazuyoshi Miura ameandika upya rekodi yake kama mwanasoka mkongwe zaidi kwa kucheza soka akiwa na umri wa miaka 55 na siku 225.

Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Japan aliingia akitokea benchi siku ya Jumapili na kufanya tukio lililovunja rekodi kwa timu ya daraja la nne ya Suzuka Point Getters.

 

Kazuyoshi Miura

Aliingia uwanjani dakika ya 76, akiisaidia timu yake kushinda 1-0 dhidi ya Criacao Shinjuku mbele ya umati wa watu 16,218 wa Ligi ya Soka ya Japani kwenye Uwanja mpya wa Taifa uliojengwa upya.

Licha ya ushindi huo, furaha kubwa zaidi ya siku hiyo iliwekwa kwa mwanamume huyo aliyepewa jina la utani ‘King Kazu‘ ambaye atafikisha miaka 56 Februari ijayo.

 

Kazuyoshi Miura

Miura alimchezea Verdy Kawasaki katika mechi yao ya ufunguzi ya Ligi ya Japan, mwaka 1993 kwenye Uwanja wa Taifa na baada ya kufumania nyavu mara nyingi kwenye uwanja huo maarufu, uchezaji wake wa kuvunja rekodi uligubikwa na hisia.

Tayari amefichua kuwa angependa kuendelea kucheza hadi atakapofikisha umri wa miaka 60 na wachache wangeweka dau dhidi yake kufikia mafanikio hayo ya ajabu.
Baada ya tukio hilo muhimu Miura alisema: “Ninashukuru kwa kucheza katika mazingira bora zaidi, na ninajisikia fahari.

 

Kazuyoshi Miura

“Nilitaka mchezo huu uwe sehemu ya historia ninayotengeneza. Baada ya kupata nafasi ya kucheza mahali kama hii, nitakuwa mnyenyekevu na kuendelea bila kusahau njaa.”

Miura kwa sasa anashika nafasi ya saba kwenye chati ya wafungaji wa muda wote ya Ligi ya Japan akiwa na mabao 139.

Acha ujumbe