Azam FC Matumaini Bado Yapo

BAADA ya kupoteza ugenini kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Al Akhadar ya Libya, Azam FC hesabu zao ni kupata matokeo nyumbani.

Wakiwa ugenini walikubali kipigo cha mabao 3-0 jambo ambalo linawafanya wawe na kibarua cha kusaka ushindi wa zaidi ya mabao matatu bila kufungwa wakiwa Azam Complex.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Denis Lavagne ameweka wazi kuwa makosa ambayo wamefanya watafanyia kazi kupata matokeo.

“Kuna makosa tulifanya kwenye mchezo wetu wa kwanza na tayari tumeshayafanyia kazi kikubwa ni kwamba tupo tayari kwa mchezo huo,”.

Tayari kikosi kimeanza mazoezi kwa ajili ya mchezo huo kuwakabili waarabu wa Libya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90 kwenye hatua ya Kombe la Shirikisho Afrika.


 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.