Kocha wa klabu ya Queens Park Rangers Michael Beale amekubali kuinoa klabu ya Wolverhampton Wanderers baada ya kufikiana makubalino ya pande zote.
Wolverhampton Wanderers baada ya kuachana na kocha wake Bruno Lage, pia walijaribu kumsajiri kocha wa zamani Julen Lopetegui lakini alikataa nafasi ya kuinoa klabu hiyo kabla ya kujaribu kuzungumza na makocha wengine zaidi.
Michael Beale mwenye miaka 42 alijiunga na klabu ya Wolverhampton Wanderers kwenye msimu wa majira ya kiangazi, lakini yuko tayari kujiunga na klabu Wolves na anatarajiwa kutangazwa kwenye viunga vya Molineux.
Wolves kwa sasa wanatarajia kuvunja mkataba wake na Queens Park Rangers ambapo wanajiandaa kulipa ada yote ili kukamilisha uhamisho huo.
Michael Beale tokea achukue mikoba ya kuoinoa Queens Park Rangers amefanikiwa kuingoza klabu hiyo mpka kwenye nafasi ya sita ya msimamo wa ligi ya Championship msimu.

