Golikipa wa Azam FC na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Aishi Manula amerejeshwa kwenye kikosicha taifa stars kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki ya FIFA Series 2026 itakayofanyika Rwanda. Taifa Stars itacheza mechi hizo Machi 26 na Machi 29, 2026, huku wachezaji wakiwajibika kuanza kambi ya mazoezi kuanzia Machi 22.
Kikosi cha wachezaji 25 kilichotangazwa na kocha Miguel Ángel Gamondi kina mchanganyiko wa wachezaji wa ndani na wachezaji waliopo klabu za kimataifa. Mbali na Manula, golikipa wengine walioitwa ni Yona Amosi kutoka Pamba Jiji na Zuberi Foba wa Azam FC.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kati ya wachezaji walioitwa, kuna wachezaji mashuhuri kama Haji Mnoga kutoka Salford City, ya Uingereza, Novatus Dismas kutoka Göztepe FC, Uturuki, Alphonce Mabila kutoka Shamakhi, Azerbaijan, na Charles M’Mombwa kutokea Floriana FC, Malta, wakionyesha mchanganyiko wa ubora na uzoefu wa kimataifa ndani ya kikosi.
Wachezaji wengine waliotajwa ni pamoja na Nickson Kibabage wa Simba SC, Bakari Mwamnyeto Yanga sc, Mohamed Hussein Yanga sc Ibrahim Abdulla Yanga sc, na wengine, wote wakiwa wamechaguliwa kwa uwezo wao wa kipekee na mchango wanayoweza kuleta katika timu.
Maandalizi haya ya kikosi cha Taifa Stars yanatarajiwa kuhakikisha timu inakuwa tayari kushindana kikamilifu kwenye michezo ya kimataifa kirafiki ya FIFA Series 2026.

