Samir Nasri Aishambulia CAF Kwa Uamuzi Tata wa Fainali ya AFCON 2025

Mchezaji wa zamani wa Arsenal FC na Manchester City, Samir Nasri, ameibuka na ukosoaji mkali dhidi ya Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kufuatia uamuzi wake tata katika fainali ya AFCON 2025.

Samir Nasri Aishambulia CAF Kwa Uamuzi Tata wa Fainali ya AFCON 2025Kamati hiyo iliamua kuipatia Morocco ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Senegal baada ya Senegal kudaiwa kujiondoa uwanjani, hatua iliyotafsiriwa kama kupoteza mechi kwa mujibu wa kanuni za mashindano. Hata hivyo, uamuzi huo umeibua mjadala mkubwa katika ulimwengu wa soka, huku wadau wengi wakionyesha kutoridhishwa nao.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Akizungumza kwa hisia kali, Nasri aliuelezea uamuzi huo kuwa wa aibu na usiozingatia haki. Alishangazwa na namna suala hilo lilivyoshughulikiwa, akidai kuwa linavunja misingi ya haki katika michezo.

Samir Nasri Aishambulia CAF Kwa Uamuzi Tata wa Fainali ya AFCON 2025

“Ni bora hata wangesubiri hadi mwaka 2035 kutangaza uamuzi kama huu. Hii ni kinyume kabisa na haki, ni upuuzi mtupu. Wachezaji wa Senegal tayari walikuwa wamerudi nyumbani na kombe wakisherehekea ushindi wao, halafu leo mnawapokonya. Sasa tufanye nini? Tulipe Morocco kombe?” alinukuliwa Nasri.

Samir Nasri Aishambulia CAF Kwa Uamuzi Tata wa Fainali ya AFCON 2025Nyota huyo wa zamani aliendelea kushambulia CAF kwa kile alichokiita maamuzi yasiyo na mantiki, akisisitiza kuwa yameharibu taswira ya soka la Afrika.

“CAF imefanya jambo lisilo na maana kabisa, ni kituko,” aliongeza.

Sakata hilo linaendelea kuzua mjadala mpana, huku mashabiki na wachambuzi wa soka wakisubiri ufafanuzi zaidi juu ya tukio hilo ambalo linaonekana kuacha doa katika historia ya mashindano ya AFCON.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.