Mbappe ana mtihani kama wa Obama jioni ile ya 2008 pale Chicago, safari ya mtoto huyu ilianzia pale visiwani Monaco kwenye dimba la Stade Louis, aliwastua Wafaransa, alibisha hodi kwenye lango kubwa la historia ya soka lao
Nachotaka kuwaambia ni kuwa taifa lile halina tabia ya kuwapamba sana watu waliofanya makubwa kwenye soka lao, sahau kuhusu Raymond Kopa, Thierry Henry na Michel Platin, hawa wote licha ya ubora wao hakuna hata mmoja aliyepewa heshma ya sanamu (statue) watu mioyo yao ya baridi tu

Sanamu pekee ni la Zinadine Zidane, ilimchukua muda msanifu Abdel Abssemed kuliandaa, lakini sio kwamba ni sanamu la kumsifu mtoto wa mitaa ya La Castallane, Marseille bali ni sanamu la kuwakumbusha vizazi kuwa Zidane alifanya ujinga kumpiga Matterazzi kichwa, tukakosa kombe kwa ujinga wake
Nageuka kuitazama miguu ya Mbappe, najaribu kuwaza atabadili upepo huu?? Ataweza kujengewa sanamu bora kukumbusha vizazi juu ya ubora wake??, Nafikiria mchezaji wa kwanza kinda kufikisha mabao 15 UEFA, nafikiria ni mchezaji wa kwanza wa akiba kupiga hatrick UEFA
Nafunua tena ukurasa nagundua licha ya miaka yake 21 ni mchezaji ghali namba mbili duniani, naendelea kufahamu kuwa ni kinda wa pili baada ya Pele kuingia kambani kwenye fainali za kombe la dunia, bado nawaza alikuwepo sehemu ya kikosi cha mastaa ila alidhihirisha ubora wake
Bado nawaza mabao yake 90 kwenye mechi 120 za PSG na assists 49 naona kuna kitu, naiona tena historia ya Mwafrika kwenye historia ya taifa kubwa kama Ufaransa, akifika miaka 28 naamini sanamu litakuwepo pale Paris! Tuombe uzima


Mwajuma
Watamkumbuka sanaa kwa mambo aliowafanyia,na history aliyoiweka
Gabriel
Mbappe anaweza kumrith zinadane kama ataendelea na uwezo wake
Magdalena
Mbappe atafata nyayo za zidane
Amani
nagundua licha ya miaka yake 21 ni mchezaji ghali namba mbili duniani, naendelea kufahamu kuwa ni kinda wa pili baada ya Pele kuingia kambani kwenye fainali za kombe la dunia Ni historia pia bado anazidi kuweka history
Emmy cleopa
Ahsante kwa taarifa
Aziza mushi
Mbappe akijitahidi atamrithi zidane
dorophina
Mbappe Ni mchezaji mzuri lazima haache historia kwa mpira wake mzuri
mathayo sonje
nafikiri ni mambo mengi ameweza kuyafanya lakini mpaka kukaa akilini mwa watu lazima afanye jambo lakipekee; kama la zizu, maana kumpiga mtu kichwa kama kile ”aiseee!!!!” si jambo la kawaida
Povel
Mbappe the best player France and Europe
David pere
History ameweka bado akiwa mdogo na haitafutika milele na watamkumbuka kwa mengi hususani kwenye timu ya taifa
Kenani
Amekuja na majabu meng kweny soccer lake lazma awakae watu kichwan
Lydia Emmanuel Magoti
Mbappe yupo vizuri razima haonyeshe mahajabu kuwakaa watu vichwani lazima kwasababu anajua nn anakifanya huyo jamaa anakubalika
Zeiyana
Mbappe mpambanaji hanayejiamini..!hatajenga history yake
Ernest
Makala nzuri sana , nimependa ulivyomchambua kijana huyu machachali kwenye soka ambapo napata mashaka kama angekuwa muingereza hiyo promo yake sasa.
mwakalosi
huyu kijana anaonekana ni hatari kulingana na ligi anayocheza ligi ya ufaransa ni moja ya ligi nyepesi sana sikushangaa chamakh kutoka kuwa mfungaji bora ufaransa kwenda arsenal sasa kiande cha mwisho
Sadick
Mbappe ni mchezaji mzuri tena bado kinda na ili kuonyesha yeye ni bora achezee ligi tofauti kuonyesha ubora alioonyesha akiwa Monaco na PSG. Ronaldo ameonyesha ubora wake katika ligi tofauti#meridianbettz
Mwanaidi
Mbappe ni mchezaji mwenye umri mdogo lakini ni mchezaji mahiri sana hasa akiwa uwanjani lazima wamkumbuke
Elika
Mbappe ni mchezaji bora sana kwa upande wangu..nategemea ataweka historia katika soka
Tahiya
Mbappe ni mchezaji mzur na kiumri bado anasafar ndefu ya kufika mbali sana katika soka natumai atajengewa sanamu muda ukifika
aisha
Mbappe anajua sana
Devotha
Mbappe mchezaji ambae hatasahaulika ujerumani hata kama wasipomjengea sanamu
Neema hassan
Mbappe mchezaji mzuri sana ,ingekuwa sahh angejengewa sanamu iwe kumbkumbu ya kudumu kwa vizazi vijavyo..
Mariam mtandama
Asante kwa taarifa meridianbet #
Rehema Dickson
Sana atakumbukwa kwa uwezo wake wa kujitoa kwa kupiga mpira na kujituma bila kujal umri wala tim kubwa kiasi gan anayocheza nayo ameonesha juhudi kubwa ni jambo zuri la kuigwa na vijana wanao chipukia katika soka hongera sana mbappe utafika mbali sana zaidi ya ulipo now
Rehema
Mbappe Ni mchezaji mzuri pia bado mdogo na ili kuonyesha yy Ni Bora zaidi acheze lingi tofauti kuonyesha ubora wake!
winfrida
lazima akumbukwe tu mbappe ni mchezaji mzuri
Warda
Mbappe kawa gumzo #Meridianbettz
Juliana
Asante kwataharifa
Hope mwaikuka
Eeh kikubwa uhai
Agness
Mbappe ni mchezaji mzuri lazima aache historia
Antony Luseno
Kwa Mbappe bado mno anahitaji juhudi za ziada maana kuna kawaida ya wachezaji wadogo kulewa hela wanazopata
Hamidu
Talent player#meridianbettz
Asha
Mbappe mchezaj mzur Sana hv sasa ulaya na dunia
felister
bonge la makala ahsanteni meridian
Neema juma
Mbappe namwamini zaidi coz ni kijana anayejitambua na anajua anachokifanya lazima aache historia
Frank Patrick
lakini akihitaji tuzo kubwa yamfaa aende Liverpool Madrid or Barca
Ester jackson
mchezaji ghali namba mbili duniani, naendelea kufahamu kuwa ni kinda wa pili baada ya Pele kuingia kambani kwenye fainali za kombe la dunia## meridianbettz
Shafii
Mbape yuko vizuri Sana anapokua dimbani anapambana kweli
Caroline
Kweli kabisa
Theonestina
Mbappe ni Yuko vizur Sana
Adelta
Mbappe anaweza kumrithi zidane
Kama akiongeza juhudi
Samiah
Mbappe atachukuwa mikoba ya zidane
Salma
Mbappe yupo vizur nafikili anaweza akamvuka hata zidane
Theckla
Mbappe namkubali sana
Hope mwaikuka
Noma sanaa huyo dogo
Ester mmakasa
Mbappe tangu nilivoanza kumsikia mpaka leo bado yuko vizuri sana yaani hashuki daraja.
Furahav
Yuko vizuri.
Issa
Bado ana muda zaidi wa kuonyesha ubora wake pale ufaransa
Fatina mfingi
Asanteh kwa taarifa meridianbet
farida ahmadi
Asante kwa taarifa