Klabu ya Yanga kupitia Kampuni ya GSM imemaliza utata sakata la kiungo wa timu hiyo, Bernard Morrison kwamba tayari ana mkataba wa miaka miwili na timu hiyo. Kauli hiyo imetolewa siku moja baada ya kiungo huyo kusikika kwenye vyombo vya habari akieleza kwamba kwa sasa yupo njia panda kufuatia kula dola 5,000 kutoka Simba, ambayo alipewa na wakala wake na ndio maana hakusafiri na timu kwenda Shinyanga.

Akizungumza Dar es Salaam kwenye kituo kimoja cha radio, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM , Hersi Said alisema anachojua mchezaji huyo ni mali hali ya Yanga, kwani bado ana mkataba wa miaka miwili ya kuendelea kuitumikia timu hiyo.
“Ninachofahamu ni mchezaji halali wa Yanga, mkataba wake wa awali wa miezi sita bado mwezi mmoja unaisha tarehe 14 Julai lakini kutokana ubora wake, tulimsainisha mkataba mpya wa miaka miwili, ambao utaanza Julai 15 na utaisha mwaka 2022,” alisema Said.
Alisema baada ya kusikia sauti ya mchezaji huyo ambaye kwa sasa hajulikani halipo, uongozi wa Yanga una njia sahihi ya kupelekea malalamiko kwenye idara husika na kuona jambo linashughulikiwa kwa haraka. Said alisema kama kuna mtu au timu inamhitaji mchezaji huyo wanapaswa kupita njia sahihi, huku akieleza sababu ya Morissoni kushindwa kusafiri na kikosi hicho kwenda Shinyanga halihusiani na masuala ya mkataba.

Morrison alieleza kwamba wakala wake alipokea dola 10,000 kutoka kwa kiongozi wa Simba, ambaye anatamani ajiunge na kikosi hicho, ambapo nusu ya fedha hiyo alipewa mchezaji huyo na nyingine amechukua wakala ili kujiunga na Wekundu hao wa Msimbazi mkataba utakapomalizika.


Issa
Ni vizuri abakie hapo yanga
Njiku
Bernard Morison nimchezaji mzuri na kila mtanzania na asiye mtanzania hanakili juu ya uwezo wake Ila yanga wasijisahau sababu uwezo wa Morison unaonekana uwanjan ndio maana simba wanamnyemelea mchezaji huyo hata alikuwa na jeuri na kibuli cha kutosha kutokusafiri na timu shinyanga
Caroline
Morrison anataka kuzingua
lombo
dah mpira wa kibongo kwel jau yan mchezaj wakimchoka yanga anachukuliwa na simba na akichoka na yanga anachukuliwa na yanga ndo nn sas kwa hali hii sidhan kama sika la bongo litasonga
Neema
Duuu hii nayo habari ngenii kwa kwelii
Salma
Safi sana
Devotha
Morrison kukijua kiswahili kidogo tu ameanza kusumbua!
Johnmary joel
Maamuzi hayo tumuachie mwenyewe#meridianbettz
felister
uyu Morris sidhan kama yupo sawa anapokeaje ela wakati hajamilizana na yanga bado…?
Magdalena
Aache kuzingua atulie tu
Sadick
Hili la Morrison linachafua hadhi ya Simba kwamba wanashindwa kufuata kanuni na taratibu za kusajiri mchezaji na Viongozi wa Yanga wanapaswa kuongelea hili sio wafadhili GSM kufanya kila kitu!#meridianbettz
Leonard
Mali ya yanga wengine watulie
Dorophina
Morison akiama kwenda simba yanga kutakuwa hamna kitu tena maana bado wanamuhitaji
Mwanaidi
Huyu ndiye Bernad Marison hanaga masiahara
Theckla
Namkubali Sana
Evaluziga
Madison namkubali sana
Genia Sikaluzwe
Daaaah hatari
Ernest
Mpira wa Bongo bhana, hizi zinaitwa figisu figisu.
Antony Luseno
Huu ni utata ambao ulikuwa unahitaji ukataji wa fitina ili ifahamike maana vyombo vya habari vilikuwa vinaongea mengi
David Pere
Bora amesaini kwenye timu ambayo Ndio iliyomleta Tanzania
Leticia
Safi
Elika
Mbona anazingua huyo morson,mala simba mala yanga mbona haeleweki
Fatuma kasomo
Simuelewagi
Sabrina
Maoni:simba wanatamaa wanamtaka Bernad marison wameona yanga wanafaidi tena
Mwanahamisi
Morrison baba lao
Gabriel
Habar njema kwetu wanayanga
isha
Yuko vizuri sana
Haulath/Lath graaffix
Morison ni 🔥
Khadija
Safi sana meridian kwa makala nzuri#meridianbettz
Hamidu
Kiungo fundi
christopher
duh sio mchezo, simba vipaji vinatosha tayar hatumuitaji huyo jamaa
Ester jackson
Safi sana Morison utaweza kuipeleka yanga mbele siku za mbeleni
Hope mwaikuka
Tatizo tamaa
Neema hassan
Asante kwa makala#meridianbettz
Povel
Morrison fundiiiii wa mpira bongo
Shafii
Morison ni mchezaji mzuri kila mmoja analifaham ilo Kama ayuko tayari kuitumikia club hiyo inapaswa afuate taratibu na Sheria za mkataba wake ukimruhusu afanye maamuzi sahihi na clubu anayo itaka kwa sasa
Frank Patrick
Pila la bongo bhana eti mchezaji anaigomea club eti na anazima simu kuwa haendi kucheza match
Mwajuma
Yanga wajipange tu wamtafute mchezaji mkali kuliko yeye ili maringo yamuishe
Zeiyana
Morison nakukubali sana ila unataka kuleta miyeyusho sasa kama unataka kusepa fuata kanuni na utaratibu wamkataba wako kama unakuruhusu sawa
Furahav
Hongera
warda
Abaki tu na yanga yake#Meridianbettz
Amani
Yanga wanapaswa kuongelea hili sio wafadhili GSM kufanya kila kitu!#meridianbett
Emmy cleopa
Abaki tu yanga #meridianbettz
Lydia Emmanuel Magoti
Yupo vizuri anajua Morison ila amalizie mkataba wake angalie ustarabu mwingine
Tatu
Morrison mzunguaji huyo