Maumivu yaliyoje kukosa nafasi ya kutazama pambano la mwisho kati ya Mohammed Alli na Joe Frazier. Lilikuwa Pambano la kusimamisha dunia, pambano la kuzima jua na pambano la kutuliza bahari.
Muhammad Alli na Joe Frazier walikuwa wanakutana kwa mara ya tatu. Frazier alishinda pambano la kwanza, Alli alishinda la pili, hili la tatu lilikuwa la kumaliza ubishi wa nani mbabe. Mara hii likifanyika mji wa Manilla, Ufilipino.

Zilikuwa zimebaki dakika 15 ifike saa tano asubuhi kengele ya kuashiria pambano lilianze ilipopigwa ndani ya Araneta Queizone. Muhammad Alli kama kawaida yake alianza vurugu zake mapema sana, akimtupia Frazier matusi kabla hata hajaanza kurusha ngumi. Joe alimchekea tu na kumwambia “Huna kitu leo”.
Alli alishinda round ya kwanza na ya pili. Akaanza kwa kasi round ya tatu akiendelea kumtukana Joe na kumuambia maneno ya kejeli kama “nipige kwa nguvu nyani wewe.. tatizo ngumi zako laini kama za mke wangu. nakuambia ntakuua leo”. Ila ni katika round ya tatu Joe alifanikiwa kuingiza ngumi ya kwanza kwa Alli.
Frazier aliendelea kumuwashia moto Alli katika round tatu zilizofuata. Alli akarejea kutawala round ya saba na ya nane. Katika round ya tisa Alli alikimbilia pembeni na kumuambia ‘corner man’ wake “ndugu yangu nakufa, kweli tena nakufa kabla sijaandika urithi”. Upande mwingine wa ulingo Joe Frazier alikuwa anaugulia maumivu ya uso uliovimba kiasi cha kumziba jicho lake la kushoto.
‘Corner man’ wa Frazier alitupa taulo ulingoni katika round ya 14, japo bondia wake alishinikiza anataka kuendelea. Baada ya pambano Joe Frazier alisema “kweli yule jamaa ni shujaa, nimempiga ngumi zinazoweza kudondosha ukuta, ngumi zinazoweza kumdondosha farasi asinyanyuke tena”.
Alli yeye alisema, “sijawahi kusogelea kifo kama leo, Frazier alikubali yaishe sekunde kadhaa kabla yangu”.


Tahiya
Ama kwa hakika lilikiwa ni pambano la haina yake mana kila mmoja halikumbana na kipigo
Frank Patrick
Dah mpaka unatamani ungekuwa kwenye nafsi ya corner wa Frazier
Omary lukumbi
Duuh hii ilikua zaid ya pambano n zaid ya vita maana si kwa matukio hayo ya kustajabisha na ngonjera zote kila mtu akiomba tukio liishe kila mmoja alijiona hafai kwa mwenzie hii kali kuliko
mwakalosi
navuta picha hili pambano lilikuwaje ngoja nikalisake nione
Fatuma kasomo
Kila mmoja alijiona hafai kwa mwenzie
Mwanahamisi
Duuh hakika pambano ili ni lakibabe
Zeiyana
Duuuh..! Yani mtu unakufa uku unajiona michezo mingine siyo poa
Rehema Dickson
Kwel huu mchezo sio poa mtu anae cheza mchezo wa ngumi muache ale pesa yake mwenyewe maana sio kwa shuruba hii
Ester mmakasa
Mapambano ulikuwa wa kipekee sana huu .
Lydia Emmanuel Magoti
Mapambano ulikuwa watari sana
Mariam mtandama
Duuuh
Caroline
Mbona mambo yalikua makubwa
Samira
Zamani mpambano ulikua wa ukweli sana
Aziza mushi
💪pambano la kibabe hakika.
neema hassan
Ile cku hakika haitoweza sahaulika kwa mashabk..
neema hassan
Ile siku hakika haitoweza sahaulika kwa mashabik
David Pere
Alli Alikuwa bondia hatari sana anapokuwa ukingoni
Sadick
Inadaiwa lilikuwa pambano la karne. Walikuwa wakweli kwamba kila mmoja alikuwa mkali#meridianbettz
Neema hassan
Hii siku haitoweza sahaulika kwa mashabki
Kenani
Pambano la kufa mtu
Magdalena
Pambano Kali Sana ili mshindi apatikane
Ester jackson
Hili pambano lilikuwa Kali sana mana hakuna aliye kubali kumpa mwezake ushindi walivumilia mpaka mwalimu wao akarusha taulo chini kuashiria kukatishwa likatishe lakini wao walipigana kiuhakika hili mbambano nilikuwa la kishujaa
Furahav
Mmh hatari sana.
Amani
walivumilia mpaka mwalimu wao akarusha taulo chini kuashiria kukatishwa likatishe lakini wao walipigana kiuhakika hili mbambano lilikuwa la kishujaa
Povel
Lilokuwah pambano la kipekeeh hlo
Neema
Aiseee hilo pambanoo lilikuwa fireeee
Ernest
Frazier amejiwekea rekodi kubwa sana kwenye ulimwengu wa masumbwi kwa kumtandika mkali wa masumbwi Muhammed Alli
Amiri Kayera
Duh kwer Ally shujaa
warda
Ila mwamedi kama mwamedi alitisha sana#Meridianbettz
Theonestina
Apo mshindi lazma apatikane
Asia Abdy
Pambano kal sana hili