
Gari hilo lililofika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar saa 2:05 asubuhi, liliandaliwa maalum kwa ajili ya wachezaji hao kupanda huku wakisherehekea ubingwa wa huo wa ligi waliouchukua kwa mara ya tatu mfululizo.
Msafara huo wa Simba ulitua kwenye uwanja wa ndege saa 3:00 asubuhi wakitokea Ruangwa, Lindi kabla ya kwenda kupanda ndege Mtwara na kuanza safari ya kurejea Dar wakitoka kucheza michezo yake miwili ya ligi na Ndanda FC, Namungo FC ambayo yote walimaliza kwa suluhu.
Baada ya kuwazuia wachezaji hao kupanda kwenye gari hilo, Sven akatoa maagizo wote wapande kwenye gari aina ya Toyota Coaster ya timu hiyo wanayoitumia U20 na ile ya wanawake.
Baadaye Sven alitoka kwenye mlango mkubwa wa kutokea abiria akiwa amekunja uso na kumfuata msaidizi wa Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa timu hiyo, Senzo Mazingisa ambaye ni Rispa Hatibu kisha akamfuata ofisa mmoja wa Simba na kuanza kumfokea kwa sauti kubwa akisikika kuonekana kugomea mapokezi hayo.
“Kitendo hicho kimeonekana kuwakera viongozi hao walioongozana na msafara huo akiwemo Kaimu Rais wa Simba, Kaduguda (Mwina) ambaye yeye mara baada ya kumuona kocha anafoka, akaachana naye akaondoka na usafiri wake,” alisema mtoa taarifa huyo.
Msafara wa timu hiyo ulianza safari ya kutoka uwanja wa ndege hapo saa 3:10 asubuhi kwa Toyota Coaster huku wakiliacha gari la wazi na kuelekea Mbweni Ndege Beach ambako timu hiyo imeweka kambi yake kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga.



Theckla
Simba wako vizuri ….!!!!
Dee
Ahsante kwa taarifa
David Pere
Wakifungwa na yanga tu saherehe zote zinakuwa chungu Mana hakuna Raha tena
Zuhura omary kindamba
Simba ni timu bora kwanza iko vizuri na wachezaji wake wako vizuri
Aziza mushi
Nawkubali sana Simba wapo vizuri ⛹️👍
mwakalosi
kocha anaogopa korona
Flomena
Simba wako gud
Leonard
Homa ya jiji jpili hiyo
Hamidu
Simba mabingwa Mara 3 mfururizo#meridianbettz
Samira
Simba ni mabingwa mara 3 mfululizo na jumapili lazima tumchape yanga
Amani
Kocha ajakosea yuko sahihi kabisa #meridianbettz
Adelta
Simba wako vizuri
Fatuma kasomo
Simba tupo vizuri yanga msubiri kichapo
Dorophina
Kumbe simba waoga wameshindwa kushangilia kisa yanga Wana wasi wasi ya kuchezea kichapo jpili
caroline
pole yao wapunguze kiranga.
mwajuma
Simba ndio mpango mzima kesho#Meridianbettz
Magdalena
Kocha anawakinga wachezaji wake na corona
Ester jackson
Haha ha haa simba toeni sababu zenu sio kisa yanga msishangilie au mganga wenu ameshaona kuwa mtafungwa achane uoga au mtoe sababu zenu mchezo kesho tusibirie nani anashinda sio mtoe lawama kisa yanga mtachekwa .
Genia Sikaluzwe
Simba mabigwa
isha
Simba mko vizuri sana
Lydia Emmanuel Magoti
Kuna nn tena huko msimbazi
Fatina mfingi
Simba ndo habar ya jiji
Tatu
Tatizo wana msimbazi ni waoga sana ishu ya jpili inawatia kimue mue
Zeiyana
Mna mbwe mbwe sana mbio za sakafuni sikuzote zinaishia ukingoni
felister
🤣🤣🤣Simba washaanza ona sintofahamu mapema
Franky
Ahahhaaaaaa….hawoookkkkk
Ester mmakasa
Safi sana Simba ila lazima viongozi wawe na mawasiliano ili kuepuka kutokuelewana mbele za watu .
Nasra
Simba wapo vzuri msimu huu
Ernest
Mechi za watani wa jadi zinakuwa na mambo mengi sana hasa nchi zetu za kiafrika
Povel tz
SIMBA soka la bongo wametawala
lombo
THIS IS SIMBA
Samiah
Simba damuni
Edgar
Matokeo huwanjani
Christa
Wasubiri dabi ipite ndo washerehekee
Rehema
Ngoja tuone matokeo uwanjani
Njiku
Simbaaa
Amiri Kayera
Hatariii
Isaya massawe
Wasi wasi wao tuu
Gabriel
Simba lazma wawe na hofu ukiangalia Kwanza wao muda huu wanafurahia ubingwa ila upande wa yanga wanapiga tiz wawe fit kwa mwenye akil ataelewe hiyo siku ikifika Simba kama atachomoka lazam kocha wao awe na hofu kubwa awez kuwa na aman
Furahav
Duuh hatari sana.
devotha
kocha anahofu sana kwa sababu mechi ya simba na yanga ni ngumu sana, kwa upande wake endapo simba akifungwa lawama zote zitakua upande wa kocha
Salma
Mh awa nao
Sadick
Hakukuwa na mawasiliano mazuri kabla , nadhani Kocha hakufanya vyema#meridianbettz
Shafii
Nomaa sanaa
warda
Simba wanatia sana raha#Meridianbettz
sabrina
Asante kwa taarifa