Utafiti uliofanywa na jarida la Forbes, umeonesha wachezaji wanawake wanaocheza mchezo wa Tennis ni miongoni mwa wanamichezo matajiri duniani.
Katika orodha ya wachezaji 10, 9 wanacheza mchezo wa Tennis wakati 1 ni mcheza soka wa timu ya taifa ya Marekani – Alex Morgan.
Wafahamu wacheza Tennis matajiri duniani.
- Naomi Osaka

Osaka anauraia wa nchi mbili lakini aliamua kuichagua kuipeperusha bendera ya Japan kwenye Michuano ya Tokyo 2020 Summer Olympic. Anamapato ya dola za kimarekani milioni 37.4. Uamuzi wake umepatia faida kubwa kibiashara ambapo anafanyakazi na makampuni yanayodhamini Michuano ya Olympic kama vile Procter & Gamble, All Nippon Airways and Nissin. Ni Roger Federer pekee anatengeneza pesa ndefu kupitia matangazo kumzidi Osaka.
2. Serena Williams

Anamapato ya dola za kimarekani milioni 36. Kupitia ushirikiano wa kibiashara na makampuni kama Nike, Gatorade, Procter & Gamble, na Beats, kunamuongezea Serena wigo wa mashabiki na kufikia milioni 40 katika mitandao yote ya kijamii – Twitter, Instagram na FaceBook. Serena na mumewe [Alexis Ohanian], ni sehemu ya kikundi cha uwekezaji kilichozawadiwa timu ya National Women’s Soccer League jijini Los Angeles- Marekani. Mtoto wake – Olympia ni sehemu ya kikundi hicho na katika umri wa miaka 2 pekee, anatambulika kama mmliki mdogo wa timu ya michezo.
3. Ashleigh Barty.

Barty anamapato ya dola za kimarekani milioni 13.1. Alishinda taji lake la kwanza katika Michuano ya French Open mwaka 2019 na kuchagiza kupata bonasi kutoka kwa wadhamini wa michuano hiyo – Fila and Head. Anamikataba ya kibiashara na makampuni kama Rado, Jaguar, Vegemite, Banana Boat na Esmi. Juni 2019, aliweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kutoka Australia kushika nafasi ya 1 toka mwaka 1976.
4. Simona Halep

Akiwa na mapato ya dola za kimarekani milioni 10.9. Halep alibeba tuzo yake ya pili ya Slam mwaka jana katika Mashindano ya Wimbledon. Anafanyakazi na wafadhili kama Nike, Wilson, Hubolt na Avon.
5. Bianca Andreescu

Anamapato ya dola za kimarekani milioni 8.9. Aliweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Canada kuwahi kushinda tuzo ya Grand Slam katika Mashindano ya US Open mwaka 2019. Ushindi huo pamoja na uzoefu wake kwa miaka 5, ulimpatia fursa ya kufanya kazi na makampuni kama Nike, Rolex, Gatorade, Royale na Sleep Country.
Katika orodha ya wachezaji wanawake 10 matajiri duniani. Wa 6 ni Garbine Muguruza (dola milioni 6.6), wa 7 ni Elina Svitolina (dola milioni 6.4), wa 8 ni Sofia Kenin (dola milioni 5.8), wa 9 ni Angelique Kerber (dola milioni 5.3) na wa 10 ni Alex Morgan (dola milioni 4.6) ambaye ni mcheza soka.
Drops and Wins!
Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.


Latifa juma mohamed
Habari njema na meridian#
gabriel
kiukwel wenzetu wanathamin sana michezo sana na pia wanaonyesha ushabk kwa kila aina michezo ambayo wanayoianzisha hiyo hufanya ushindan wenye faida sana ukiangalia
Theonestina
Ni kwer
Sabrina
Duuh kumbe nilikua sifahamu Asante kwa kunijuza
farida ahmadi
Habari njema Sana
Issa
Habari njema kwa hili
Samiah
Nihabari njemaa
Mwajumah
Ni habari njema sana
rama
Maoni:sawa kabisa
Nasra
Asante kwa taarifa
Zeiyana
Kwenye tasnia ya michezo wenzetu wanajitaidi sana
Mwanahamisi
Asante kwa makala
gabriel
ukweli usiopingwa
Magdalena
kabisa tennis inachezwa sana na matajiri na nchi za wenzetu wamekuwa wakiupa kipaumbele sana huu mchezo
Ester jackson
Kweli kabisa wanaongoza hazina ubishi
Lydia Emmanuel Magoti
Nikweri kabisa mchezo usio pingwa nawatu na upendwa na watu
Furahav
Daah tennis kumbe mchezo mzuri sana.
Christa
Dahhh, wana hela nyingi
David Pere
kiukwel wenzetu wanathamin sana michezo sana na pia wanaonyesha ushabk kwa kila aina michezo ambayo wanayoianzisha hiyo hufanya ushindan wenye faida sana ukiangalia
Theckla
Asante kwa taarifa