National Football League (NFL) ni ligi ya mpira wa miguu wa Amerika ya Kaskazini ambayo inajumuisha jumla ya timu 32 ambapo kilele cha mchezo huo huwa ni Super Bowl. Kuelekea msimu mpya wa NFL ambayo itaanza kutimua vumbi Septemba 9 tumekuendalia timu kubwa zenye nguvu 10 kabla kaunza kwa ligi hiyo.

- Tampa Bay Buccaneers: Mabingwa watetezi wa Super Bowl mara zote wamekuwa wakifungua katika nafasi ya kwanza sababu ya ubora wao na usitarajie kama wataondoka katika nafasi hii kwa msimu wote.
- Buffalo Bills: Hii ni timu yenye vipaji lukuki ambavyo vina silaha na uwezo wa kufunga katika eneno la ufungaji, Na eneo la ulinzi litakuwa vyema vilevile, ndiyo maana imewekwa katika nafasi ya pili.
- Kansas City Chiefs: Uundwaji upya mzuri wa safu ya ushambuliaji utairejesha Chiefs katika njia yao ya ufungaji alama kubwa na Patrick Mahomes akiiwasha. Kuna wasiwasi juu ya ulinzi ambao unapaswa kuboreshwa.
- Green Bay Packers: Aaron Rodgers amerudi. Kwa kuwa baba mwenye nyumba yupo, Basi Packers ni timu tena inayoweza kushinda vikali. Lakini pia hii ni timu nyingine ambayo inapaswa kupiga hatua kwenye safu ya ulinzi ili kufikia Super Bowl.
- Cleveland Browns: Ukizungumzia kuhusu vipaji vipo hapa sasa ni muda wa kuwa na matarajio mazuri unapo waona. The Browns ni timu inayopewa nafasi kubwa ndani ya AFC North na wapo hapa kwa sababu.
- San Fransisco 49ers: Haijalishi ni nani anacheza robo ya nyuma(quaterback), hii ndio timu nadhani itashinda NFC West. Jimmy Garoppolo ni kama ataanza msimu, lakini Trey Lance atakuwepo pia. Wapo vyema tena, Jambo ambalo ni habari mbaya kwa daraja lote.
- Baltimore Ravens: Suala kubwa ni kama mchezo uliyopita ataboresha vya kutosha msimu huu. Lamar Jackson ni silaha yao madhubuti, lakini mchezo unaokuja anapaswa kuwa bora zaidi kushinda yote.
- Los Angeles Rams: Matt Stafford analeta kawaida yake ya kufanya mauaji katika safu ya ufungaji. Hilo ni jambo zuri. Ulinzi unapaswa tena kuwa bora zaidi, ndiyo sababu wengine wanachagua Rams kuwa timu Bora.
- Arizona Cardinal: Wameongeza baadhi ya wakongwe J.J. Watt na A.J Green wameonyesha kuwa ni wakati wa kucheza kwa dhati kabisa. Huu ni msimu mkubwa kwa kocha Kliff Kingsbury.
- Tennesse Titans: Wanapaswa kufunga sana na silaha zao Derrick Henry na Julio Jones wakijumuishwa kwa hiyo ni suala la ulinzi kufanyiwa kazi katika timu hii, walikuwa dhaifu msimu uliyopita wanapaswa kuimarika ili waweze kushinda taji la daraja.
Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.


