Giannis Antetokounmpo Amewekahistoria NBA.

Kabla ya msimu mpya wa NBA kuanza kutimua vumbi Disemba 22, 2020. Giannis Antetokounmpo wa Milwaukee Bucks ameweka historia kwenye NBA.

Giannis Antetokounmpo ameongezewa mkataba wa kuendelea kukipiga katika klabu ya Bucks ambao unathamani ni pauni milioni 170.1, huu ni mkataba wenye mtonyo mrefu zaidi kwenye historia ya NBA.

Antetokounmpo amesaini mkataba wa miaka 5 na wakala wake alithibitisha thamani ya mkataba huo kupitia ESPN ambapo sasa ni rasmi, mchezaji huyu ambaye ameshabeba tuzo ya MVP mara 2 amempiku James Harden ambaye aliweka rekodi 2017 kwa mkataba wenye thamani ya pauni milioni 169.9

Antetokounmpo Akipambana na wachezaji wa Miami Heats.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Antetokounmpo ameandika “Hapa ni nyumbani, huu ni mji wangu. Nimebarikiwa kuwa sehemu ya Milwaukee Bucks kwa miaka 5 zaidi. ”

Endapo Giannis Antetokounmpo asingesaini mkataba huu, angekuwa ni mchezaji huru baada ya msimu wa 2020-21. Mkataba mpya wa mchezaji huyu unamruhusu kuvunja mkataba huu baada ya kuutumikia kwa miaka minne.


BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!

INGIA MCHEZONI!

16 Komentara

    NBA mambo yanazidi kunoga

    Jibu

    NBA mambo yanazid kupamba moto

    Jibu

    NBA Mambo nimoto

    Jibu

    Nba Mambo yanazidi kutalaladi

    Jibu

    Safi sanaaa

    Jibu

    Habari njema kwa mashabiki wa giannis kuongezewa mkataba

    Jibu

    He did a gud job

    Jibu

    Historia safi na rekod ya kibabe

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Safiii sana

    Jibu

    NBA kumenoga

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Good

    Jibu

Acha ujumbe