Ngoma ngumu kunako fainali ya Eastern Conference kwenye NBA. Jimmy Butler akataa utumwa mbele ya Boston Celtics.

Celtics waliingia uwanjani wakiwa wanaongoza kwa matokeo ya 3-2 baada ya michezo 5 kati ya 7. Ni ushindi 1 tu waliuhitaji ili kutwaa taji la ubingwa wa Eastern Conference mbele ya Miami Heats. Mchongo umeungua, Jimmy Butler awa kirusi.

Butler ameokoa jahazi la Heats baada ya kupachika jumla ya pointi 47 kwenye mchezo wa 6 na kuwa sehemu kubwa ya ushindi wa pointi 111-107 kwa Heats. Uhondo wa kumsaka bingwa wa kanda ya mashariki unaendelea na, kwa matokeo haya, bingwa tajulikana kwenye mchezo wa 7.

Usiku wa kuamkia Jumanne wiki ijayo ndio mtanange wa maamuzi utachezwa. Ni Butler au Tatum atakayekwenda kuchuana na Curry kwenye fainali ya NBA msimu huu?


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

 

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa