Msimu mpya wa NBA – 2020/21 unaendelea kushika kasi siku baada ya siku, rekodi zinawekwa na kuvunjwa kila wiki. LeBron James na Becky Hammon wameweka zao wiki hii.
LA Lakers walikuwa uwanjani kupambana na San Antonio Spurs. Mchezo ambapo Lakers wameshinda kwa pointi 121-107, LeBron James alikuwa anasherehekea miaka 36 ya kuzaliwa kwake.
Pamoja na kusherehekea siku kuu yake ya kuzaliwa, LeBron ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kwenye historia ya NBA kufunga ‘double-digits’ mara 1,000.
James alipachika pointi 26 na sasa amevunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Michael Jordan. Mara ya mwisho kwa James kushindwa kumaliza mchezo wa kufunga mwaka kwa kufunga pointi 10 au zaidi ilikuwa Januari 5,2007.
Mchezo wa Lakers vs Spurs ulikuwa na tukio lingine la kihistoria ambapo kocha msaidizi wa Spurs – Becky Hammon amekuwa kocha wa kwanza mwanamke kuongoza timu kwenye ligi ya NBA.
Hammon alichukua majukumu ya kocha mkuu wa timu hiyo – Gregg Popovich ambaye alitolewa uwanjani baada ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?
Tatu
NBA kazi ipo
Sabrina
NBA 🔥
Adelta
NBA wanajitambuwa sana
Shakila mrope
NBA ni watu makini san
Fatina mfingi
Nice
Ernest Kimeru
LeBron kaanza mabalaa yake
Caroline
Inabidi wajitaidi maana walishuka kiwango
warda
NBA ya sasa hivi imepoa sana
Dorophina
NBA lazima kieleweke
Angelina
NBA kumenoga
Rahmal
Nba kumepamba moto
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif meridianbet
Sarah
Mambo ya NBA hayo
Sania
NBA kumenoga
Hopemwaikuka
Mambo yametarad