Bondia mkongwe Floyd Mayweather amefunguka kiu yake ya kutaka kumsajili bondia huru Terence Crawford baada ya mwanamasumbwi huyo kumaliza kandarasi yake na Top Rank mwaka uliyopita.
Akiongea na Ben Thompson Mayweather alizungumzia kuhusu kutaka kumshika mkono Mmarekani mweusi mwenzake.
Alisemea: “Hakuna tofauti Mchina anamsaidia mchina, Wadominiki wanasaidia Wadominiki, Wamexico kwa Wamexico mimi ni Mmarekani mweusi ningependa kusaini Wamarekani Weusi kwanza nimekuwa nikimuhitaji bondia machachari Terence Crawford.
“Tumeongea kwenye hafla kadhaa tunaongea pia kwenye simu kila mtu ana namba ya mwenzake. Nimeongelea kuhusu Crawford kupata mapambano anayoyataka”.
Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.