MSHAMBUIAJI wa Yanga, Fiston Mayele ameweka rekodi kwenye mashindano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kufunga hat trick mbili.

Mayele ameweka rekodi hiyo jana jumamosi ambapo timu yake ilikuwa ikimenyana na Zalan FC kwenye hatua ya awali ya michuano hiyo.

mayeleYanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 kwenye mchezo huo wa marudiano ambapo mabao yalifungwa na Farid Mussa, Stephan Aziz huku Mayele akifunga mabao matatu.

Mayele ameweka rekodi kwenye hatua ya awali ya michuano ya Klabu bingwa barani Afrika ambapo katika michezo miwili amefanikiwa kufunga jumla ya mabao sita.


Katika mchezo wa kwanza dhidi ya Zalan Mayele alifunga mabao matatu huku Yanga ikifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Baada ya kuwatoa Zalan Yanga watakutana na kati ya St George ya Ethiopia au Al Hilal ya Sudan katika hatua inayofuata ya ligi ya mabingwa barani Afrika.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa