Bale Aipeleka Wales Fainali ya Mchujo Kufuzu Kombe la Dunia

Mchezaji Gareth Bale alifunga mabao mawili katika ushindi wa 2-1 wa Wales dhidi ya Austria katika mchezo wa nusu fainali ya mchujo katika kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 64.

Bale Aipeleka Wales Fainali ya Mchujo Kufuzu Kombe la Dunia

Bale ambaye ameichezea Real Madrid michezo mitano pekee kati ya 42 kwenye michuano yote msimu huu na jumla ya dakika 270 uwanjani alikosekana katika El Classico ambapo Barcelona iliinyuka Real Madrid 4-0.

Gareth Bale amekuwa katika  kiwango kizuri na timu ya taifa akifanikiwa kufunga jumla ya mabao 5 katika michezo minne.

Wales wataumana na Scotland au Ukraine mchezo wa fainali ya mchujo mchezo ambao utaamua nani anasonga mechi ambayo itapigwa katika uwanja wa nyumbani kwa Wales.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe