Caballero Afunguka Tofauti ya Tuchel na Lampard

Golikipa wa Chelsea Willy Caballero ameelezea tofauti zilizopo kati ya kocha wa zamani wa Chelsea Frank Lampard na bosi wa sasa Thomas Tuchel akiwa ametumia muda wake kuwa na makocha hao.

Caballero Afunguka Tofauti ya Tuchel na Lampard

Tuchel alichukua mikoba kwa Lampard mwezi Januari baada ya kiungo huyo wa zamani wa Chelsea kufukuzwa kufuatia kuwa na muelekeo mbaya wa timu.

Caballero amesema Tuchel anatofauti sana kuliko mtangulizi wake hasa kwenye soka la kisasa.

“Kimsingi kuzungumzia kuhusu makocha, kuwa mmoja amefanya vizuri na mwingine amefanya vibaya sio jambo zuri,” Caballero aliiambia 90min, “kwa sababu wote wameitumika Chelsea kwa sababu ya kitu, ni kwasababu wote ni walimu wazuri wanaushawishi kwenye soka.

“Bila shaka tulipokuwa na Lampard tulikuwa na mawazo ya moja kwa moja hasa kwa soka la Kiingereza, kushambulia haraka, mashambulizi ya pembeni na katikati kushambulia na umaliziaji wa kutokea katikati lakini pia alipenda counter-attacking.

“Sasa na Tuchel, anatumia mbinu ya kucheza kwa pamoja, kumiliki mpira, tunatengeneza nafasi nyingi mara nyingi amekuwa akituambia jinsi ya kuendeleza na kuwasoma wapinzani sehemu gani ni muhimu, kwa maana ya uimara wao na udhaifu wao.

Tuchel tangu achukue mikoba ya kuinoa Chelsea mwezi Januari ameshinda michezo 10 na kutoa sare mechi 4 katika michezo 14 ya Premier League na kwasasa Chelsea wamekaa katika nafasi ya nne kwenye msimamo.


Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

7 Komentara

    Caballero yupo sahihi tuchel yupo vizuri

    Jibu

    Duuh

    Jibu

    Hatari

    Jibu

    Ni kweli

    Jibu

    Wote wako vizuri

    Jibu

    Nomaa

    Jibu

    Tuchel ni mzoefu

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.