Spurs Wanamtaka Kulusevski Mazima

Klabu ya Tottenham Hotspurs hawataki kusubiri mpaka miezi 18 ipite ili waweze kumpa mkataba wa kudumu Dejan Kulusevski kama ilivyoainishwa kwenye kipengele cha mkataba wao wa sasa wa mkopo kinacho ruhusu kumnunua moja kwa moja.

Spurs Wanamtaka Kulusevski Mazima

Mchezaji huyo wa Sweden tayari amekuwa na msaada kwenye timu ya Conte akifanikiwa kufunga mabao 2 na kutoa asisti tano tangu alipo jiunga na klabu hiyo mwezi Januari mwaka huu.

Kulusevski alitua katika klabu hiyo London akitokea Juventus kwa dili ya mkopo ya mwaka mmoja na nusu lakini kiwango cha kuvutia alichoonyesha katika michezo kadhaa aliyocheza mpaka sasa klabu hiyo inataka kusajili moja kwa moja wakati wa usajili wa kiangazi kwa dau la paundi milioni 25.

Mchezaji huyo wa miaka 21 alitua Spurs pamoja na mchezaji mwezake Rodrigo Bentacur wakitokea Juventus wameisadia Tottenham kuwa na matumaini ya kumaliza top four msimu huu.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe