Nyota wa Real Madrid Toni Kroos amesema anampango wa kustaafu akiwa na klabu ya hiyo ya LaLiga.

Toni Kroos Anataka Kustaafia Real Madrid

Kroos amefurahia mafanikio mbalimbali makubwa tangu ajiunge na Madrid akitokea klabu ya Bundesliga Bayern Munich mwaka 2014, na kufanikiwa kushinda mataji kama Champions League tatu na LaLiga mbili pia akifanikiwa kupata mataji mengine 13 ya heshima.

Mchezaji huyo wa miaka 31 amecheza mechi 309 kwa Real madrid katika mashindano yote na anakua Mjerumani alicheza mechi nyingi zaidi kwa kumpita Uli Stielike.

Kroos amefanikiwa kufunga mabao 21 tangu atue katika klabu ya Madrid aliiambia Madrid TV: “Ni kitu maalumu, unapoangalia Wajerumani ambao wamecheza hapa unagundua kuwa wanamajina makubw: Gunter Netzer, Bernd Schuster au Stielike.

“Kumpita Stielike ambaye ni gwiji katika klabu, inanifanya niwe na furaha sana, ni rekodi maalumu nina jivunia kufikia hatua hii.

“Kama nisemavyo siku zote, wazo langu ni kustaafia hapa na hicho ndiyo ninaenda kukifanya.”

Kroos amefunga mabao mawilina kutoa asisst sita katika michezo 22aliyocheza katika LaLiga msimu huu, wakati amecheza mechi 31 kwenye mashindano yote.

Madrid wapo nafasi ya 3 katika LaLiga wakiwa nyuma ya Majirani zao Atletico kwa tofauti ya alama tano kuelekea mchezo wa Madrid Derby siku ya Jumapili.


Ni Muda wa Kuvuna Mkwanja na Jungle Jim and the Lost Sphinx

Hauihitaji kufikira mara mbili ni mchezo gani utakupatia mkwanja ndani ya kasino za Meridianbet. Jiunge sasa ufurahie Jungle Jim and the Lost Sphinx.

Kroos, Toni Kroos Anataka Kustaafia Real Madrid, Meridianbet

  CHEZA HAPA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa