KUELEKEA siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi, Uongozi wa Yanga umetembelea shule ya Sekondari ya wasichana Jangwani na kukabidhi zawadi mbalimbali.

Hiyo ni moja kati ya ratiba zilizopo ikiwa ni kuelekea siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi ambayo itafanyika Agosti 6 mwaka huu.

Yanga, Yanga Yatembelea Shule ya Jangwani, Meridianbet

Akizungumzia hilo, Rais wa klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa hiyo ni moja ya shamra shamra kuelekea katika kilele cha wiki ya mwananchi.

“Tumefurahi sana kuwa hapa Jangwani na tunaona asilimia kubwa ya wanafunzi wa hapa ni mashabiki wetu hivyo muendelee kutusapoti na sisi tupo nanyi.

“Hizi ni shamra shamra kuelekea siku ya kilele cha wiki ya mwananchi hivyo kuna mambo mengine yataendelea kufanyika kuelekea huko.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa