Wajerumani wnaa msemo wao maarufu sana unaosema “ Nur die Harten kommen in den Garten” ambao una maana “ wenye nguvu pekee ndio hushinda vita au kufika mwisho kishujaa “
Mshindo Msola aliichukua Yanga SC ikiwa hoi taabani kiuchumi na kisoka . Aliikuta Yanga katika kipindi ambacho haikuwa na hata uwezo wakuwa na uhakika w akilipa mishahara ya wachezaji kwa miezi mitatu mbele.
Mshindo Msola
Mshindo Msola

Timu ilifikia hatua ya kutembeza bakuli ili ijimudu kiuchumi mbele ya vilabu ambavyo vilitopea kwenye ukwasi, Simba SC na Azam FC. Washindani.

Msola alikuja na ahadi ya kuweka BILIONI MOJA klabuni , kauli ambayo ilionekana kituko cha mwaka na siasa za soka .

Kauli yake ilikuwa kituko kwakuwa wengi walipima uwezo wake kiuchumi na kusahau kuipima akili yake, busara na hekima , ujuzi kiungozi, maarifa na ushawishi mbele ya vyanzo vya uhakika vya kiuchumi. Dokta alikuwa mbele yao kiakili akiwaacha nyuma wakicheka kwa husuda.

Mshindo Msola kwanza kabisa akaanza na stratejia za kuwakumbusha wanachama thamani ya klabu yao na kuwapa mtihani wa kuona ugumu wa kuendesha klabu pasipokuwa na mikakati kabambe ya kiuchumi. Akaleta bakuli ili kila mmoja ajikamue ( ownership ) . Hii ikafeli.

Mshindo Msola
Mshindo Msola

Baada ya huo mtihani kwa wanachama na yeye kufanikiwa kuwaonesha mfumo wa ujima ulivyo mgumu kuendesha klabu , akaenda kwenye phase two ya mkakati wake ambao mabilioni yake yalipokuwepo.

Kwanza akaweka task force ya vijana wengi wasomi na wenye maono ya mbali katika soka la kisasa lenye kuweka mizani sawa ya UCHUMI na SOKA.

Baada ya hapo akafungua milango kwa wawekezaji na hapo ndipo GSM na wengine wakaingia na kumwaga yale mabilioni .

Msola akakaa chini tena akaona pesa bila mkakati wa leo na kesho yatakuwa yale yale ya zile zama za TUMIA UWEZAVYO KESHO NITAKUPA TENA.

Mshindo Msola
Mshindo Msola

Hapa ndio akaibuka na mikataba mirefu ya kimkakati kwa wawekezaji na mikakati yakuijaza klabu na watu wenye taaluma sahihi sehemu husika. Hapa unawaona kina Senzo Hammilton Mazingiza na ile timu ya wanasheria pale klabuni

“ najua ipo siku utakuwa kiongozi wa Yanga . Umekuwa vyema sana kwenye scouting ya wachezaji na mikakati ya ushindi “ ni kauli ya Msolwa akiongea na Eng Hersi . Hapa utaona alikuwa na leadership strategy

Imeandikwa na Samuel Samuel.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa