Nabi Awaomba Msamaha Mashabiki Yanga

Benchi la ufundi la Yanga likiongozwa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi limewaomba msamaha mashabiki wa klabu hiyo kutokana na timu kutoonyesha kiwango bora kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

Yanga walicheza mchezo huo wa ligi jana jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Clement Mzize.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Nabi aliwapongeza wapinzani wao Kagera Sugar kutokana na mchezo mzuri waliouonyesha.

“Kwanza tunashukuru tumepata pointi tatu ni jambo la muhimu zaidi kwetu kwani mipango yetu ni kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

“Wachezaji wetu walikuwa wamechoka hivyo tuliangalia wale ambao wanaweza kucheza katika uwanja kama huu, tunashukuru tumepata pointi tatu.

“Tunawaomba msamaha mashabiki wetu kutokana na kiwango kisichokuwa kizuri leo na hiyo imetokana na ratiba kutubana hivyo wachezaji wamechoka.”

Acha ujumbe