Benitez: Lucas Digne Ilikuwa ni Biashara Nzuri

Kocha wa timu ya Everton Rafael Benitez amesisitiza kwamba kuondoka kwa Lucas Digne ni biashara mzuri kwa klabu yake ya Everton.

Mlinzi huyo wakushoto kutokea taifa la Ufaransa amejiunga na klabu ya Aston Villa kwa uhamsho uliogharimu kiasi cha £25milioni baada ya kupoteza matumaini akiwa chini ya Benitez kwenye viunga vya Goodison Park.

Benitez

Benitez alinukuliwa akisema, “ni jambo zuri, kumbadilisha mchezaji ambaye alikuwa anafikisha miaka 29 na wachezaji vijana, mimi ni kocha na nawajibuika na maamuzi yangu, ni muda wakuifikilia timu na mipango ya baadae, inabidi tusonge mbele.”

Digne ambaye amesaini mkataba wamiaka minne na nusu na klabu ya Aston Villa alisema kuwa hakutarajia kuondoka kama alivyoondoka kwenye viunga vya Goodison Park huku akimtuhumu kocha wake.

“Ni mtu mmoja wa kutoka nnje ambaye ataharibu mapenzi yako” alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe