Kocha wa klabu ya Ajax Erik ten Hag amefikianana makubaliano na klabu ya Manchester United ya kuwa kocha wa klabu ya hiyo baada ya msimu kuisha japo hakuna maandishi yoyote yaliowekwa kuhusu makubaliano na inaaminika kuwa ni makubalino ya maungumzo tu ndiyo yaliofanyika.

Ajax wanatambua kuwa kocha wao amefanya makubaliano na klabu ya Man Utd, na bado kuna makubaliano ambayo wanahitaji kumalizia ya kusainishana nyaraka, wakati bado hakuna makubaliano yoyote yaliondikwa wala kutangazwa, inatarajia kuwa baada ya Dutch Cup final kati ya Ajax dhidi ya PSV Ten Hag atatangaza hatma yake.

Erik ten Hag anatarajiwa kuchukua mikoba ya kuinoa klabu ya Man Utd, kupokea kijiti cha aliyekuwa kocha wa muda Ralf Rangnick ambaye anakwenda kwenye majukumu yake kuwa mshauri wa timu.

Sio klabu ya Manchester United wala upande wa Erik ten Hag ambao wamekubali kuthibitisha kuwa kuna mazungumzo ya makubaliano ambayo wameyafanya.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa