Hiannick Kamba Amepatikana Akiwa Hai Baada miaka 4

Hiannick Kamba 🇨🇩 apatikana tena Baada ya Kutangazwa Kufariki Katika Ajali ya Gari Mnamo mwaka 2016. Mchezaji wa zamani wa klabu ya Schalke 04, Hiannick Kamba amepatikana akiwa hai nchini Ujerumani ikiwa ni miaka minne baada ya kutangazwa kuwa amefariki katika ajali ya gari.

Hiannick-Kamba


Mnamo Januari 2016 Kamba aliripotiwa kupata ajali ya gari akiwa nchini kwao Congo na klabu yake ya wakati huo, VfB Huls, ilisema kwamba mchezaji huyo alikuwa amepoteza maisha kwenye ajali hiyo. Kamba ambaye kwa sasa ana miaka 33, ameripotiwa kupatikana akiwa hai katika jiji la Ujerumani la Gelsenkirchen na anaweza kukabiliwa na mashtaka ya kisheria.

Mwendesha mashtaka Anette Milk amefunguka kuwa kesi inachunguzwa dhidi ya mke wa zamani wa Kamba, anayedaiwa kukusanya ‘malipo ya bima ya maisha’ ya mchezaji huyo mara tu baada ya kuripotiwa kifo chake. Anette ambaye ni Mke wa zamani wa mchezaji huyo alidai kuwa anastahili malipo ya bima ya maisha ya mchezaji huyo mara tu alipopata habari ya kifo na alionyesha hati ya kifo kwa kampuni ya Bima.

Bild imeripoti kuwa Kamba atakuwa kama sehemu ya ushahidi katika uchunguzi juu ya udanganyifu ulioweza kutokea. Beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Congo, aliwahi pia kucheza na kipa Manuel Neuer wakiwa katika klabu ya Schalke, pia alichezea vilabu vya Ujerumani kama SV Zweckel, SG Borken na Recklinghausen wakati wa maisha yake ya soka.

MCongo huyo kwa sasa anafanya kazi kama Mtaalam wa kemikali kwenye kampuni ya usambazaji wa nishati

12 Komentara

    Duh! Asante meridian kwa habari hii

    Jibu

    thnks meridian kwa habari moto moto za kimichezo

    Jibu

    Habar ya kushangaza inamaana alizikwa akiwa hai? Au mistake

    Jibu

    Aisee kumbe hakufaa kijana wa watu. Taarifa tunazipata huku meridianbet

    Jibu

    Du kumbe ajafa nashukuru kulifaham hvyo

    Jibu

    Inauma sana kusingiziwa kifo

    Jibu

    Du inashangaza sana

    Jibu

    Daah!inasikitisha Sana…lkn aliwezaje kupata Cheti Cha kifo?

    Jibu

    Duu isee hii habari nzito

    Jibu

    duh Mambo yapo meridian

    Jibu

    Inasikitisha sana.

    Jibu

    Duuuh mwanamke anatamaa sana.najiuliza amewezaje kupata hati ya kifo😲

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.