Aaron Ramsey Afunga Goli Lake la Kwanza Dhidi ya Celtic

Mchezaji anayechezea kwa mkopo kwenye klabu ya Rangers Aaron Ramsey ameifungia timu hiyo goli lake la kwanza tokea asajiriwe kwenye dirisha la usajiri la mwezi january na klabu hiyo akitokea klabu ya Juventus.

Mahasimu wao ndizo klabu pekee ambazo zinzchuana kwenye kinyanganyiro cha ubingwa wa ligi kuu ya Scotland, ambapo kabla ya mchezo kuanza kulikuwa na tofauti ya alama tatu huku celtic akiwa anaongozwa kwa alama 76 dhidi ya Rangers ambaye alikuwa na alama 73.

Aaron Ramsey alitumia dakika tatu kuweza kuiandikia goli lake la kwanza timu yake, huku akipokea pasi safi kutoka kwa Ryan Kent na kumalizia kwa ustadi mkubwa na kuifanya Rangers kuwa mbele kabla ya mambo kubadilika na mchezo kuisha kwa Rangers kupoteza kwa goli 2-1.

Celtic ilitumia dakika nne tu kuweza kusawazisha goli lililofungwa na Aaron Ramsey, kupitia kwa Tom Logic aliyemalizia mpira uliokolewa na golikipa wa Rangers, dakika ya 43  Carter-Vicker alimaliza ndoto za Rangers kwa kufunga goli la pili kabla ya mapumziko na kufanya mpira uishe kwa goli 2-1.

Kwa sasa Celtic wako kileleni kwa alama sita zaidi ya Rangers ambao wanashika nafasi ya pili.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe