Bayern Wataadhibiwa Kuchezesha Wachezaji 12?

Klabu ya Bayern Munich iliibuka na ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya Freiburg siku ya Jumamosi na kujikita kileleni mwa Bundesliga lakini kuna makosa yalitokea wakati wa mchezo.

Bayern Wataadhibiwa Kuchezesha Wachezaji 12?

Katika dakika ya 86, Corentin Tolisso na Kingsley Coman walitolewa nje ilinafasi zao zichukuliwe na Marcel Sabitzer na Niklas Süle. Ni Tolisso pekee aliyetoka, na kuiacha Bayern ikiwa na wachezaji 12 kwa sekunde 17.

Kulingana na Sky kabla ya wachezaji kumuarifu mwamuzi Christian Dingert kuhusu suala hilo. Mchezo huo ulisimama kwa dakika nane, na mazungumzo makali kati ya viongozi wa Bayern na mwamuzi yalifanyika kabla ya usawa kurejeshwa. Wakati huo, Bayern walikuwa wameshinda 3-1.

Dingert anasema suala hilo lilitokana na makosa ya meneja wa timu ya Bayern, Kathleen Krüger, ambaye alionyesha nambari isiyo sahihi ya mchezaji kwenye ubao wa kielektroniki. Wakati Süle alipoingia kwenye nambari 29 namba ya zamani ya Kingsley Coman ilionyeshwa badala ya namba 11 namba ya sasa ya Coman, na kumwacha Mfaransa huyo bila kujua kwamba alipaswa kutoka.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe