Hazard Anena Juu ya Lukaku, Sarri na Conte

Aliyekuwa nyota wa Chelsea, Eden Hazard ambaye sasa anatarajia kupeta sana kwenye Ligi ya La Liga akiwa na Real Madrid, amenena mambo kadhaa kuhusu aliyekuwa nyota wa Man United Romelu Lukaku na mameneja wake wa zamani pale Chelsea Antonio Conte na Maurizio Sarri.

Nyota huyu raia wa Ubelgiji alikamilisha uhamisho wake kwenda kwenye klabu ya ndoto ya zake. Akizungumza na jarida la Corriere della Sera anasisitiza kuwa hii ilikuwa ni ndoto toka alipokuwa mtoto.

“Tangia nilipokuwa mtoto, niliota ndoto kuwa siku moja nitavaa jezi ya Real Madrid. Real Madrid wakikugongea mlango wako, unaweza kufanya kitu kimoja tu, kuufungua.” -Hazard

Licha ya kufanikiwa kuhamia klabu yake mpya, anasema ana kumbukumbu za kudumu za Chelsea, pia Hazard ameutambua mchango wa walimu wake waliopita Conte na Sarri akiwa klabuni Chelsea

“Nimejifunza mambo mengi sana kutoka kwao. Wote wako tofauti sana, utu wao na mitazamo yao juu ya soka, lakini wanafanana kitu kimoja. Wote ni mabingwa!” -Hazard

Lukaku pia amekamilisha uhamisho wake toka United akitua Inter Milan wakati dirisha la uhamisho likielekea ukingoni kwa ada ya paundi milioni 65. Hazard amemzungumzia staa huyu, namna anavyo mfahamu na matarajio yake akiwa Inter Milan.

“Lukaku ni mshambuliaji mzuri, mfungaji anayeweza kuendana na timu nyingi, anafunga magoli mengi, kitu ambacho ni muhimu zaidi kwa kiungo mshambuliaji, lakini liakuwa ni kosa kumzungumzia kwa kipimo hicho tu. Anafanya mambo mengi pia.” -Hazard

2 Komentara

    Kipindi hicho alikuwa yuko vizuri ila kwa sasa kiwango keshuka bora arudi Chelsea tu

    Jibu

    Alikuwa yupo vizuri kwasasa ameyumba Sana

    Jibu

Acha ujumbe